Wednesday, March 7, 2012

Airtel Tanzania yadhamiria kuboresha huduma kwa wateja


Airtel Tanzania, mtandao unaoongoza kwa gharama nafuu na wenye wigo mkubwa Tanzania leo umezindua programu ya kuwawezesha wafanyakazi wake kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora Tanzania. Hii inakuja baada ya ya uzinduzi mzuri wa chuo cha masoko kilichozinduliwa mwezi wa kumi mwaka jana inayojulikana kama " Airtel Centum Sales University (ACSU)" Akiongea katika uzinduzi wa programu hii ya mafunzo kwa timu zinazotoa huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel ,Mkurugenzi wa Airtel Tanzania bwana Sam Elangalloor alisema,"Leo tunazindua rasmi mafunzo ya huduma kwa wateja Tanzania inayoashiria dhamira yetu katika kuleta mabadiliko na kuwaopa wateja wetu huduma bora na zenye viwango vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.lengo letu ni kuhakikisha tunatoa huduma ambazo zinazidi matarajio ya wateja wetu na kudumisha mahusiano ya muda mrefu. Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa uteja, Adriana Lyamba aliongeza kwa kusema, " mafunzo haya ni muendelezo wa kuonyesha ni kwa jinzi gani kampuni na nembo yetu inajali wateja wake.Katika siku 365 zijazo wafanyakazi wa Airtel katika kityengo cha huduma kwa wateja watajifunza mbinu za kitabia na zile za kikazi katika kutoa ufanisi zaidi na kuwaongezea ujuzi zaidi. Leo Tanzania zaidi ya wafanyazi 99 wa kitengo cha huduma kwa wateja wataanza mafunzo haya ya huduma kwa wateja katika ofisi za Airtel makao makuu Programu hii ya Airtel service Academy inatolewa na kampuni ya ukufunzi ijulikanayo kama Centum learning na itahakikisha watoa huduma wa Airtel wanakua bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment