Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 6, 2012

BONDIA Wladimir Klitschko ameweka rekodi ya kushinda mechi 50 kwa KO


BERLIN, Ujerumani
baada ya kutetea ubingwa wake wa uzito wa juu kwa kumtwanga raundi ya nne, Jean-Marc Mormeck.

Mpiganaji huyo raia wa Ukraine bingwa wa WBA, IBF na WBO alionekana kuwa katika kiwango cha juu kwa uchezaji katika pambano la upande mmoja lilichezwa mwishoni mwa wiki ESPIRIT Arena mjini Dusseldorf.

Kwa mujibu wa Sky Sports Klitschko alimmiliki mpinzani wake kabla ya kummaliza kwa ngumi kali ya kushoto baada ya kufika dakika ya 10.

Mormeck, ambaye ni bingwa zamani wa uzani wa cruiser ambaye alipigwa na David Haye mwaka 2007, alisema kabla ya pambano kuwa ataingia ulingoni bila ya kuwa na mashaka lakini hakuonekana kama aliamini kuwa angeweza kumalizwa mapema.

Badala ya yake Klitschko alitawala mechi na kuboresha rekodi yake na kuwa 57-3, huku akishinda mechi saba kwa kumaliza raundi zote ulingoni.

Klitschko alianza vya pambano hilo kwa nguvu huku akibadilishana ngumi na mpinzani wake.

Katika raundi ya pili ilionekana wazi kuwa Mormeck alikuwa na wakati ngumu dhidi ya mpinzani wake ambapo aliangushwa baada ya kupata konde la mkono wa kulia.

Mormeck alinyanyuka lakini mashabiki kiasi cha 50,000 waliona dhahiri kuwa ilingumu kwake kumaliza vizuri.

Klitschko aliendeleza mvua ya ngumi raunsi ya tatu ambapo alitupa makonde mchanganyiko, licha ya kwamba alionywa na refa kwa kumsukuma Mormeck na kumwangusha.

Shughuli iliisha raundi ya nne ambapo ngumi yua mkono wa kulia ilitua kwa Mormeck ambapo alionekana kulewa kabla ya kuanguka jukwaani.

Baada ya kuanza kuhesabiwa Mormeck alijaribu kunyanyuka lakini refa, Luis Pabon alimaliza pambano ili kuepusha madhara zaidi kwake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...