Mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJ CleoKutoka nchini Afrika ya Kusini akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu
J.K.Nyerere usiku huu, tayari kwa onyesho lake litakalofanyika kwenye viwanja
vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam siku ya Machi 10, 2012 siku ya
jumamosi, Mwanamuziki huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake wa FACEBOOK na
ameongozana na wanamuziki wenzake wawili ambapo FULLSHANGWEBLOG imeshuhudia
kuwasilia kwake.
Mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJ CleoKutoka nchini Afrikaya Kusini akisalimiana na Mkurugenzi wa Times FM Radio
Rehure Nyaulawa ambaye ndiye mwenyeji wake wakati alipokuwa akipmokea kwenye
uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere.
Mwanamuziki Tlou Cleopas Monyepae maarufu kama DJCleo Kutoka nchini Afrika ya Kusini katikati akiongozan na wanamuziki wenzake
kwenda kupanda gari tayari kuelekea hoteli ya Protea ambako ndiko
walikofikia.
No comments:
Post a Comment