Thursday, March 15, 2012

kampuni ya tigo yatoa msaada wa kompyuta 48 chuo kikuu UDOM

Tigo imetoa msaada wa kompyuta 48 kwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kama sehemu yakuboresha sekta ya elimu na kusaidia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano(Tecknohama). Hafla ya makabidhiano hayo imefanyiakaleo katika chuo kikuu cha Dodoma. Kompyuta zilikabidhiwa kwa niaba ya Tigo namratibu wa Promosheni na Matukio Bwana Edward Shila. Akizipokeakwa niaba ya chuo,kaimu makamu mkuu mipango, fedha na utawala, Prof.S.A.K.Mlacha ameshukuru Tigo kwa msaada huo na kusema kuwa kompyuta hizozitasaidia kuboresha mahitaji ya Tecknohama chuoni hapo. “Ili tuweze kukabiliana na ushindaniduniani,wanafunzi wanahitaji kuwa na uelewa juu ya kompyuta na tecknohama,”alisema Prof. Mlacha. “Msaada huu utawaunganisha na taarifa na tecknolojia kamanjia ya kusoma na kupata taarifa ya yale yanayoendelea katika masomo yao,”alisema. Bw. Shila alisema, “Teknolojia imekuwani sehemu kubwa ya maisha yetu, elimu na kazi. Tigo imefurahia kutoa komputa navifaa vingine kwa viongozi wetu wajao.” Msaada huu ni muendelezo wa msaada wavitabu, vilitolewa katika fani ya uhandisi,udaktari na fani nyinginezo ,ambavyovilikabidhiwa katika chuo kikuu cha Dodoma Desemba mwaka jana na kuhifadhiwa katika maktaba tano za chuohicho. Kuhusu Tigo: Tigo ni mtandaowa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biasharamwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wahali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemuya MillicomInternational Cellular S.A(MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu nainayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini. Msingi wamafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharamanafuu, Uwepo na Upatikanaji.Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu,zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikishakwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kulikozote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar. Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz Imetolewa na:Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501

No comments:

Post a Comment