Monday, March 5, 2012

KAWE JOGGING CLUB YAZINDULIWA LEO ASUBUHI:







KLABU ya Jogging ya Kawe imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha washiriki wa klabu zingine za maeneo mbalimbali ya jiji hilo, Kulikua na Vijana wa Temeke, Kunduchi, Taifa Biafra, Sotojo na wengine wengi. UJUMBE ULIOKONGA NYOYO ZA WATU ULIKUWA "JOGGING NDIYO LOLIONDO YA KWELI". Wadau wamepongeza juhudi za kuanzishwa kwa vikundi hivyo na kusema vitasaidia kupunguza wagonjwa mahospitalini kwani afya ya jamii itaimarika kupitia mazoezi.

Wanachama wa kawe klabu wakiwa kwenye mazoezi maeneo mbalimbali jijini Dar leo asubuhi.



Klabu Zingine za Jijini nazo zilialikwa kushiriki uzinduzi huo.



Wakikatiza Kona ya Cocacola kuelekea Kawe.



Vijana wa Temeke Jogging nao walinogesha kwenye uzindujzi huo.

Wakiwa Tanganyika Pekaz wananyoosha viungo baada ya Safari ya kilometa 12 ambapo zaidi ya watu 200 walishiriki mazoezi hayo.

3 comments:

  1. Kawe Jogging tunatarajia kuadhimisha sherehe ya kuzaliwa mwezi wa kumi katika viwanja vya Tanganyika Perkaz, tarehe 14/10/2012. Hivyo basi Clubs zote za Dar es Salaam zitahudhuria Tamasha hilo kubwa la aina yake.
    Imepostiwa na Mratibu Kawe Jogging.
    Lazaro E Ngimba.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Ilipendeza sana, hasa kwa kumwalika kiongozi wa serikali Naibu Waziri wa Sheria na Katiba (Mb)Angela Kariuki. Nilipata faraja alipozungumza na kutuasa kuhusu kuanzisha SACCOS na VICOBA. Hongereni sana wana Kawe Jogging, karibuni pia kwenye Bonanza letu tarehe 4/11/2012. Katibu Mkuu - Biafra Sports Club

    ReplyDelete