MAADHIMISHO MIAKA 10 YA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA YAFANA
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, akifurahia tuzo maalum aliyozawadiwa baada ya kuwa msimamizi wa karibu na wa moja kwa moja wa mfuko huo katika miaka ya mwanzo hasa wakati makundi mengi yalikuwa yanapinga.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akizindua kitabu cha taarifa za mfuko huo vijijini zilizokusanywa na wanahabari katika mikoa mbalimbali nchini. Kushoto ni Ofisa Habari na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael.Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakionesha vitabu viwili vilivyozinduliwa jana kikiwemo cha kuelezea maendeleo ya mfuko huo. Watumishi hao walishiriki kuhariri vitabu hivyo.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa mfuko huo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkapa Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wilson Mukama akipokea tuzo Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya NHIF, Profesa Lucian Msambichaka akipatiwa tuzo na Mizengo Pinda Rais mstaafu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Mjumbe mstaafu wa Bodi ya NHIF, Margareth Sitta akipatiwa Tuzo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema (kulia) alikuwa ni miongoni wa viongozi waalikwa. Mmiliki wa Blog maarufu ya Michuzi, Muhidin Issa Michuzi, akipatiwa tuzo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya baada ya kuwa mmoja wa mashujaa waliosaidia mfuko huo kusonga mbele Michuzi akionesha tuzo hiyo. Michuzi hivi sasa ni Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais Faraja Kihongole wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya kwa kutambua mchango wa kihabari wa kuendeleza mfuko huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF, Deogratias Ntukamazina (kushoto) akipokea tuzo kwa kuendeleza vizuri mfuko huo
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya (kushoto) akimkabidhi tuzo maalum, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Emmanuel Humba kwa kutambua mchango wake mkubwa ikiwemo kutokata tamaa alipokuwa akishambuliwa na wadau waliokuwa wakipinga kuanzishwa kwa mfuko huo.
Ntukamazina (kushoto akipongezana na Humba baada ya kukabidhiwa tuzo Picha ya pamoja ya mashujaa wa mfuko huo waliokabidhiwa tuzo Wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini, wakipata maelezo kuhusu mfumo wa kisasa wa kuhifadhi mafaili ya wateja wa NHIF Wageni waalikwa wakioneshwa jinsi mafaili yalivyopanwa kwa mpangilio mzuri Wageni waalikwa wakiangalia mafaili yanayoandaliwa kutunzwa kwa njia ya kisasa Mafaili yakipangwa vizuri ili yahifadhiwe kisasa zaidi
No comments:
Post a Comment