Friday, March 16, 2012

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI YAZINDULIWA RASMI MJINI IRINGA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christina Ishengoma akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakati alipotembelea katika banda la kampuni hiyo katika uzinduzi wa wiki ya maji inayofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa kuanzia leo Machi 16 ambapo imeelezwa kwa yatafungwa na Mh Dk.Rais Jakaya Kikwete Machi 22. Kampuni ya bia ya Serengeti ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo yakiwa na kauli mbiu ya "Maji kwa usalama wa Chakula", katik picha katikati ni Meneja wa Mahusiano ya Umma Nandi Miwyombela.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengoma akihutubia wakati wa iringa katika ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengoma akipata maelezo kutoka kwa Hamdar Chanzi Mkemia mwandamizi Maabara ya maji Iringa, kushoto ni Amani Mafuru Kaimu Mkurugenzi wa Maji vijijini Wizara ya maji na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi maadhimisho ya wiki ya maji.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengoma akikata utepe kuzindua rasmi maonyesho ya wiki ya maji kwenye uwanja wa Samora Mkoani Iringa leo, kushoto ni Amani Mafuru Kaimu Mkurugenzi wa maji vijijini Wizara ya maji.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengomaakipokea taarifa ya maadhimisho wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji kwenye uwanja wa Samora Mkoani Iringa leo, kutoka kwa Amani Mafuru Kaimu Mkurugenzi wa maji vijijini Wizara ya maji.
Kutoka kushoto ni Elias Amani Afisa wa mauzo (SBL) Imani Lwinga Meneja Mawasiliano (SBL) Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL na Nandi Mwiyombela Meneja Mahusiano ya Jamii wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionyesha baadhi ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
Hivi ndivyo vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo kama vunavyoonekana hapa
Kutoka kulia ni Bw. Timbe Mkuu wa mahusiano kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Imani Lwinga kutoka (SBL) na Nandi Mwiyombela kutoka (SBL)
Wadau mbalimbali wamejitokeza mna kutembelea banda la Kampuni ya bia ya Serengeti kama wanavyoonekana katika picha.
Maadamano yakiingia katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Wananchi mbalimbali wakiingia kwa maandam,ano katika uwanja wa Samora.
Kundi la burudani ya Tarumbeya likiongoza maandamano hayo.
Mabanda mbalimbali wakiwa tayari kwa maonyesho.
Watoto pia wameonekana wakipita katika mabanda na kujionea mambo mbalimbali kuhusu maonyesho ya maji.
Makampuni mengi yanayojishughulisha na sekta ya maji yamejitokeza ili kuonyesha bidhaa zao kama unavyoona mabanda yakiwa na matanki ya maji.

No comments:

Post a Comment