Sunday, March 11, 2012

MDAU WA NGUMI ATOA ANGALIZO LA SHERIA KWA NGUMI ZA KULIPWA


Kupambanisha boxers zaidi ya mara tatu ni makosa kisheria, hapa kwetu tunafanya kwa kutojua sheria au kwa mapromoter kutengeneza pesa. Wadau tumeliona ilo na tukiendelea kukaa kimya tutalitia aibu Taifa.
International fight zote zinaruhusu re-match na grand final after re-match, mfano Manny Pacquiao vs Erick Morales game ya kwanza alipigwa Many paquiao kwa points, akaomba re-match akashinda Manny Pac kwa KO round ya kumi. Elick Morales akaomba grand final re-match akapigwa KO round ya 3, akataka tena re-match sheria zikambana mpaka leo anataka kurudiana na Manny Pac ila walishamaliza three times fighting.
Mfano mwingine Manny Pacquiao vs Juan Manuel Marquez game ya kwanza draw, ikaja re-match akashinda Manny pac kwa points, Marquez akaomba grand final re-match ikapigwa akashinda Manny pac kwa pints ilikua very close fight, mpaka leo wanataka re-match ila sheria za boxing zinawabana haiwezekani tena.
Riddic Bowe vs Evender Holifield zimepigwa three times, moja draw mbili alipigwa Evander, na Evander alitaka re-match ikashindikana kwa kuwa walishamaliza zile three times fighting na awawezi kupigana tena. Na mifano mingi tu ila hiyo michache inatosha.
Hapa kwetu tumeshuudia boxers wakipigana zaidi ya mara saba na watu kwa kutojua sheria wanaona ni jambo la kawaida ila ni makosa kisheria, vyama vyetu vya ngumi PST, TPBO, TPBC ect, baadhi vinajua hilo na baadhi havijui hilo kabisa. Ni makosa kupiganisha watu zaidi ya mara tatu.
Rashid Matumla vs Maneno Osward wamepigana zaidi ya mara 5 au 6 na bado wanataka kupigana tena je hapo sheria zinafutwa au wanatubuluza???????
Francis Cheka vs Rashid Matumla wameshapigana zaidi ya mara 4 na bado kuna plan ktk mwaka huu kuwapiganisha tena.
Mada Maugo vs Francis cheka, walipigana PTA akapigwa Maugo, akaomba re-match zikapigwa Morogoro Jamuhuri akapigwa tena Maugo, sasa wameingia ktk grand final zitapigwa tena April tunaomba game hii iwe ya mwisho kwao la sivyo tutawashtaki mapromoter na chama chochote kitakachotoa kibali kwa ajiri ya fight nyingine baada ya hii ya April.
Mbwana Matumla vs Francis Miyeyusho wameshapigana mara tatu wameshamaliza ila wanataka kuandaliwa pambano la nne, je ni sheria zipi zinazofuatwa hapo.
Vyama vya ngumi za kulipwa walitazame hili kwa makini mkubwa sana tena sana, kama sheria awazijui basi waulize au waingie ktk mitandao waangalie na kufuatilia International fight na sheria zake, sio kubuluza watu na huku wanafanya madudu.
Naomba kuwakilisha!
Mdau wa boxing

No comments:

Post a Comment