Thursday, March 22, 2012

RAIS JAKAYA AWASILI KWENYE UWANJA WA SAMORA MJINI IRINGA, TAYARI KWA KUFUNGA MAADHIMISHO WIKI YA MAJI


Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa Samora tayari kwa sherehe za ufungaji kilele cha sherehe za wiki ya maji zinazofanyika mjini Iringa leo, maadhimisho hayo yaliambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wadau wa Wizara ya maji, maadhimisho hayo yalikuwa yamedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL pamoja na ITV na Radio One.
Hapa akielekea jukwaani kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa maji Vijijini Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw Amani Mafuru.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa maji Vijijini Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bw Amani Mafuru mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Samora asubuhi ya leo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma akitoa salamu za Mkoa mbelea ya Rais Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa Chjama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa Bw. Deo Sanga "Jah People" akicheza ngoma ya Kibati kurtoka Zanzibar na wanakikundi cha ngoma cha Jeshi la Kujenga taifa JKT Msanii wa Mmashaili anayekwenda kwa jina la Mpemba Asilia kutoka Pemba akiimba shairi lake mbele ya Rais Jakaya Kikwete na wananchi kwa ujumla katika kilele cha maadhimisho hayo.
Wananchi walioshiriki katika maadhimisha hayo wakiwa kwenye uwanja wa Samora leo asubuhi.
Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji Nandi Mwiyombela kutoka kampuni ya bia ya Srengeti SBLa kiwapa maelezo wadau Agela na Vero walipotembelea katika banda la kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akipozi kwa picha na Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji Nandi Mwiyombela kutoka kampuni ya bia ya Srengeti SBL

No comments:

Post a Comment