Friday, March 16, 2012

MILIONI 26 KWA YA KUCHANGIA MADAWATI KUPITIA TIGO TUCHANGE

Tigo Tuchange yachangia madawati ya shule
15 Machi, 2012, Dar es Salaam. Zaidi ya watu wapatao mia moja walishiriki katika matembezi ya kujitolea katika ufunguzi wa kampeni ya Tigo Tuchange kwa ajili ya kukusanya hela ya kuchangia sekta ya elimu nchini Tanzania. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Mh. Shukuru Kawambwa alizindua matembezi hayo Machi 3, 2012, kwa kukata utepe na kuwaongoza watembeaji kutoka Shekilango Millenium Bussiness Complex hadi Ubungo mataa. Nchini kote, maelfu ya watu walijitokeza na kuongeza muda wa maongezi kupitia Tigo Rusha ili kuchangia kampeni hii.
" Ningependa kuwashukuru wote walioshiriki kuchangia kampeni ya mwaka huu" alisema Bw. Diego Gutierrez, ambaye ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kampuni ya Tigo. " Tunafuraha kufahamu kuwa matokeo ya juhudi zetu za pamoja zitaleta mabadiliko kwa mamia ya watoto wa shule nchini" alisema.

Shiling milioni 26 zimekusanywa kupitia muda wa maongezo ulionunuliwa kupitia Tigo Rusha Kati ya saa tano na saa sita mchana wa siku hiyo. Wateja walionunua muda wa maongezi kati ya muda huo, waliweza kutumia muda wao wa maongezi kama kawaida wakati Tigo ilirudufu kiasi hicho na kuingiza katika kampeni hiyo ya uboreshaji wa Elimu. Fedha zote zilizopatikana katika tukio hilo zitapelekwa kwa Hassan Majaar Trust (HTM), programu endelevu yenye lengo la kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa kutoa madawati kwa shule mbalimbali zenye uhitaji.
Mwenyekiti wa HTM, Balozi Mwanaidi Maajar, alisema "Tumefarijika sana na kampeni hii na tungependa kuwashukuru Tigo kwa mchango huu utakaosaidia mahitaji ya elimu kwa watoto wa Tanzania. Msaada huu tulioupata leo utatumika katika kununulia madawati kwa shule mbalimbali ambazo tunazo na tumethibitisha kuwa na uhitaji. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati. Tunaona kwamba hii ni hatua kubwa katika kufikia malengo yetu".
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.tigo.co.tz/

No comments:

Post a Comment