Saturday, March 10, 2012

KAMPUNI YA TIGO YATOA MSAADA WA BAISKELI KWA WAJASILIAMALI WALEMAVU



Taarifa kwa vyombo vya habariMpango wa kijasiraamali waTigo wa kuwanufaisha wenye ulemavu10 March, 2012, Dar es salaam. Tigo imetoa msaada wa baiskeli za walemavu ishirini na tano kwachama cha wajasiriamali waishio na ulemavu kama sehemu yake ya kusaidia afya katika jamii.Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo katika shule ya Buguruni ya wenye ulemavu wa kusikia, nabaiskeli hizo zimekabidhiwa kwa niaba ya Tigo na mratibu wa Promosheni na Matukio bwana EdwardShila ambapo zilipokelewa na na katibu mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation Bibi Ester Mkwizukwa niaba ya chama.“Tuna furaha kuweza kukisaidia kikundi hichi cha watu wanaoishi na ulemavu ambapo sasa kwa kutumiabaiskeli hizi wataweza kufanya shughuli zao za kijasiriamali kwa uraisi zaidi. Vile vile tunafurahakuwatambulisha katika nafasi kubwa ya biashara ya kuwa wakala wa Tigo Rusha na Tigo Pesa” alisemaBw. Shila. “tunaamini msaada wetu utasaidia kuboresha maisha yao kwa kuwaongezea uwezo wakujiongezea kipato” alisemaTigo pia inajitolea kutoa mafunzo ya kijasiriamali katika huduma zake za Tigo Rusha na Tigo Pesakwa wanachama wa chama hicho. Ushirikiano huo ni sehemu ya mpango wa kijasiriamali ambapowanachama watapata simu,kadi za simu na mafunzo kutoka Tigo. Mpango huu unatarajia kutoa msaadakwa wanachama wengine ishirini na tano Arusha na Dodoma.“Watu wanaoishi na ulemavu wanakabiliana na hali ngumu ya uchumi kuliko makundi mengine katikajamii” alisema bibi Esther Mkwizu. Tunaamini kwa kuwawezesha haitawasaidia tu kuweza kufanyashughuli zao lakini pia itawawezesha kujipatia kipato,ukizingatia kwamba ulemavu siyo kigezo chakutoweza kufanya kazi.Kampuni nyingine pia zimeshauriwa kujiunga na mpango huu na kuwasaidia watu wanaoishi na ulemavuvifaa vitakavyo wawezesha kujitegemea wenyewe.Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandaowa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemuya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuuna inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibukaAfrika na Amerika ya Kusini.Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepona Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kilamahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuukuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment