Friday, March 16, 2012

WANAWAKE 6 WAFUZU MAFUNZO YA UMEME WA JUA, INDIA

ErastoT. Ching’oro- Msemaji Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Mapema mwezi septemba, 2011, wanawake sita kutoka Wilaya ya Mtwara 94) na Lindi (2) walichaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Ufundi wa Kuunganisha Umeme Juan a Matengenezo katika Chuo cha Barefoot kilichoko nchini India kwa muda wa miezi sita. Mafunzo hayo yamehitimishwa na wanawake walioshiriki mafunzo hayo wamerejea siku ya Ijumaa tarehe 16 Machi, 2012.

Wanawake hao sita ni Esha M. Mwangana Fatina M. Mzungu (Lindi); Amina H. Nachingulu, Arafa M. Halfani, Mariam I. Luwongo, Sofia h. Mnandi na Amina H. Nachungulu (Mtwara); ambao walipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bibi Judith Kizenga, na Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchni Tanzana Bibi Anna Falk- Collins ambao waliongozana na maafisa wengine.

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na UN Women kwa ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na kupatiwa msaada wa kiufundi chini ya Mpango aw Kutoa mafunzo wa Serikali ya India nchini Tanzania. Mpango wa Chuo cha Barefoot India wa kuwajengea uwezo “Wanawake Vijijini Kuimulika Afrika” ni sehemu ya program ya utekelezaji wa mpango wa Un Women katika kusaidia maendeleo ya wananawake nchini Tanznaia.

Un Women ni sehemu ya Shirika la Umoja wa Mataifa ambalo utekeleza shughuli zake chini ya mpango wa kuendeleza mazingira na kukuza uwezo wa kiuchumi kwa wanawake. Mfunzo haya kwa wanawake mafundi wa umeme jua unalenga kutoana fursa za elimu kwa wanawake ili kukuza shughuli zao za kiuchumi na kuongeza vipato kwa maslahi ya maisha yao na familia kwa ujumla.

Mpango huu unaendeleza ujumbe maalum wa Kamati ya Hali ya Wanawake na Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani wenyekaulimbi inayosema kuuwa “Wawezeshe wanawake Vijijini; Ondoa Njaa na Umaskini”.

Baada ya mafuzo hayo ya miezi sita wakufunzi wanaofuzu uhandisi wa umeme jua kutoka Chupo cha Barafoot wanatarajiwa kurejea katika vijiji vyao na kuanzisha miradi ya kuweka umeme jua katika majumbani, na watawajibika kufanya matengenezo ya mitambo hiyo kwa kwa kipindi cha miaka mitano.Wahandisi wa umeme jua wa Chuo cha Barefoot wana nia thabiti ya kudumisha na kuendeleza teknolojia ya umeme jua vijijini.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Chuo cha Barefoot na serikali ya India ina mpango wa kuanzisha kituo cha kutoa mafunzo ya umeme jua kwa wanawake wa vijijini katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya wilaya ya Mtwara vijijini ili kusambaza taaluma hii katika familia nyingi zaidi.

No comments:

Post a Comment