Friday, March 9, 2012

WAZIRI MALIMA AIBIWA HOTELINI MOROGORO

Adam Kighoma Malima

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adamu Kighoma Malima amekombwa vitu vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 katika hoteli ya kitalii ya Nashera ya mjini Morogoro.


Taarifa za kipolisi zilizopatikana kutoka mjini Morogoro zimethibitisha kutokea wizi huo zikisema ulitokea usiku wa kuamkia leo.


Zilimkariri Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman taarifa zilmesema wizi umetokea wakati waziri huyo alipokuwa amejipumzisha kwenye sebule ya chumba chake kwenye hoteli hiyo hadi mida ya 10.45 ndipo alibaini kuibiwa vitu hivyo baada ya kurudi chumbani.


Kwa mujibu wa polisi zimeibwa fedha taslimu Dola 4000 za Marekani na Sh. milioni 1.5, pete mbili za silva zenye thamani ya sh. milioni 2, simu zenye thamani ya sh. milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya sh. 50,000, laptop mbili zenye thamani ya sh. milioni 5.6, taperecorder na headphone vyote vya sh. milioni moja.


Polisi wanasema dirisha la aluminium la chumba cha hoteli alimokuwa Malima limekutwa limevunjwa kwa kitu kigumu.


Habari zinasema nje ya dirisha hilo zimeoneka nyayo nje na ndani ya chumba jambo linaloashiria kuwa ni za mwizi.


Kufuatia wizi huo, walinzi watatu wa hotel hiyo wanashikiliwa na polisi huku taarufa zilizopatikana baadaye tukiandaa kurusha ripoti hii zikisema kwamba baadhi ya vitu vilivyoibwa vimepatikana, ingawa havikutajwa.

No comments:

Post a Comment