)Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Filbert Bayi akizungumza
katika uzinduzi wa kampeni ya sababu bilioni za kulithamini bara la
Africa iliyoandaliwa na Kampuni ya Cocacola ambapo Bayi alisema kuwa
kuna haja ya watanzania kuonyesha uzalendo wa nchi yao na kuithamini
Africa, Uzinduzi huo umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani
City uliopo jiini Dar es Salaam.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Meneja mkazi wa masoko kampuni ya Cocacola Bw. Dimej Olaniyan akifafanua
kuhusu kampeni hiyo ambapo alisema kuwa kampeni hiyo itadumu kwa miaka
miwili na inalengo la kuinua yale mazuri yanayo onekana katika bara la
Afrika.
Meneja wa masoko kampuni ya Cocacola Bi.Salome Mabirizi akielezea muhimu wa kuwa na Kampeni hiyo.
Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Bw. Filbert Bayi Pamoja
na)Meneja mkazi wa masoko kampuni ya Cocacola Bw. Dimej Olaniyan
wakipata kiburuisho cha soda ya Coca cola.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika kampeni hiyo.
Mmoja wa waandishi wa habari kutoka katika Gazeti la Mwananchi
(katikati) Nora Damian aliyejinyakulia zawadi ya Televisheni
akikabidhiwa zawadi yake na Meneja mkazi wa masoko kampuni ya Cocacola
Bw. Dimej Olaniyan (kulia) kushoto ni Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki
Tanzania Bw. Filbert Bayi.
No comments:
Post a Comment