Sunday, April 22, 2012

Francis Miyeyushokizipiga Uingereza tarehe 27 mwezi


Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imetoakibali kwa bondia wa kimataifa wa Tanzania Francis Miyeyusho kucheza pambano langumi nchini Uingereza. Miyeyusho atazipiga na bondia Luke Wilton wa Uingereza tarehe 27 mwezi huu katika hoteli ya Holiday Inn iliyo katika mtaa wa jijiniBelfast, Ireland ya Kaskazini. Mpambabno huo ni wa kugombea mkanda wa kimataifawa Masters katika uzito wa Super Fly.

Miyeyusho anatarajia kuondoika nchini tarehe 22 mwezihuu siku ya Jumapili na shirika la ndege la Uingereza (British Airways).

Francis Miyeyusho ni bondia wa kimataifa aliye kwenyeviwango vya mashirikisho / vyama mbalimbali ya / vya ngumi duniani. Shirikishola ngumi la Kimataifa IBF limemweka kwenye nafasi ya 5 katika orodha yamabondia 15 bora wa mabara duniani.

Hii ni mara ya kwanza kwa Francis Miyeyusho kuchezanchini Uingereza na mabondia wa huko na anatagemea kuonyesha umahiri mkubwakatika mpambano huo.

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamtakiasafari njema Miyeyusho katika safari yake ya kuitangaza Tanzania katika medaniya michezo ya kimataifa.

Ikumbukwe kwamba ni Ngumi za Kulipwa pekee ambazozimekuwa zinaig’arisha na kuitangaza vyema Tanzania katika miaka ya karibuni.

Katika mpambano huo, wimbo wa Taifa la Jamhuri yaMuungano wa Tanznaia utapigwa mbele ya maelfu ya watanzamaji pamoja namamilioni wengine ambao watakuwa wanaangalia kwenye luninga.

TPBC imeanzisha rasmi mkakati wa kutumia mchezo wangumi za kulipwa kuitangaza Tanzania kama sehemu salama ya kufikia kwa wataliina wawekezaji (destination market for tourism and direct investments)"Sports Tourism" kwa maana ya "Utalii wa Michezo"

Aidha tunamuombea mungu Miyeyusho aende salama naafanikiwe kurejea na mkanda wa International Masters nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment