Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom 
Tanzania  Bw. Rene Meza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari 
hawapo pichani katika hafla fupi ya kukabidhi fedha kwa mshindi wa pili 
wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya  M-pesa  Bw. Revocatus Mkama 
(kulia) anaejishughulisha na ufundi wa magari jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom 
Tanzania Bw. Rene Meza (kushoto) akimkabidhi mshindi wa pili wa droo 
kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-pesa Bw. Revocatus Mkama (kulia) fedha
 taslimu shilingi milioni kumi  katika hafla fupi iliyofanyika katika 
Makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini dar es salaam.
Mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi
 ya promosheni ya M-pesa Bw. Revocatus Mkama ambaye pia ni mkazi wa 
Mwanza anayejishughulisha na ufundi wa magari akifurahia kitita cha 
shilingi milioni kumi alizoshinda kupitia promosheni ya M-pesa mara 
baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom 
Tanzania Bw. Rene Meza.
Mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-Pesa Bw. Revocatus Mkama leo amekabidhiwa kitita chake cha Shilingi 10 Milioni.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amempongeza mshindi huyo 
wakati akikambidhi kitita chake hicho kufuatia kuibuka mshindi katika 
droo ya Aprili iliyochezeshwa hivi karibuni. “Ninajisikia furaha kubwa 
kukukabidhi fedha hizi ulizoshinda ikiwa ni matunda ya kutumia hudiuma ya ”Alismea Bw. Rene.
“Wewe ni mteja mwenye bahati kubwa miongoni mwa mamilioni ya wateja wa Vodacom M-Pesa,
 nakupongeza sana na tunaimani kwamba fedha hizi zitakusaidia kubadili 
maisha yako kiuchumi.” “Azma yetu, tunataka kuona kwamba kila mmoja ana 
mudu kutumia huduma hii na huku wateja wetu wakiwezeshwa kadri watumiavyo huduma waipendayo ya M-Pesa”Aliongeza Bw. Rene
Hadi kufikia leo, zaidi ya wateja 7000 wameshajishindia jumla ya shilingi Milioni 370 wakiwemo washindi wawili wa droo ya mwezi. “Matumizi
 ya M-Pesa yameongezeka sana tangu kuanza kwa promosheni hii, tumeshusha
 gharama za huduyma hiyo na watu waendelee kutumia huduma hii bora na 
wawezeshwe.”Aliongeza Bw. Rene
Huduma ya Vodacom M-Pesa
 ndio huduma inayoongoza soko katika huduma za kibenki kupitia simu ya 
mkononi ikiwa na mtandao mpana zaidi wa mawakala zaidi ya 20,000 nchi 
nzima. “Udhati wetu katika kuhakikisha huduma hii inaendelea kuwa bora, 
salama, ya uhakika na zaidi yenye gharama nafuu kwa watu wote bila 
kujali uwezo wa kiuchumi bado ipo pale pale.”Amesisitiza Mkurugenzi 
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene. 
Kwa
 upande wake Bw. Mkama ambae ni mkazi wa Mwanza anaejishughulisha na 
ufundi wa magari jijini humo pamoja na kuishukuru Vodacom pia 
ameipongeza kwa kuleta huduma bora inayowawezesha watanzania kufanya 
miamala kupitia simu za mkononi.
“Hakuna shaka yoyote kwamba huduma ya Vodacom M-Pesa
 inaongoza soko na inatumiwa na wananchi walio wengi kama sio kutuma 
basi kupokea fedha, na hii imeipeleka nchi mbele katika matumizi ya 
teknolojia ya simu ya mkononi.”Alisem,a Bw. Mkama
Bw.
 Mkama ni mshindi wa pili droo hiyo, wa kwanza alikuwa Konstebo wa 
Polisi James Peter Mlalo, aliyeibuka mshindi katika droo ya Machi mwaka 
huu. 
Ili kuwa katika nafasi ya kushinda shilingi 50,000 kila siku , mteja wa Vodacom anatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa. Kadri mteja anavyoitumia huduma hiyo ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya kushinda zawadi ya kila siku na ile ya mwezi.
Kupitia huduma ya M-Pesa mtu huweza kutuma na kupokea pesa, kulipia na kununua gharama mbalimbali ikiwemo LUKU, DAWASCO,DSTV, Pia huduma ya M-Pesa
 hutumika kutoa na kuweka fedha katika akaunti ya mteja iliyo katika 
benki ya CRDB, kununua tiketi za safari za ndege za Precision Air, 
Coastal n.k
No comments:
Post a Comment