Wafanyakazi wa mfuko wa bima wa afya NHIF wakiwa mazoezini katika viwanja vya shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es salaam.
Hapa wakifanya mazoezi ya kukimbia kuzunguka uwanja wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es salaam.
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa
watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa
mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku
kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa kwa
sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.
Akizungumza
wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya
msingi Oyesterbay Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha
rasilimali watu na utawala bi Jane nchimbi alisema 'Tumekuwa na
utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa
tumebanwa na majukumu ,lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuufanya
utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa
ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa umma tunatumia muda mwingi kwenye
ofisini tukihudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi
kama ambavyo NHIF tumethubutu...
Mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi za
Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi
(Gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.alisema Bi Jane kijazi
Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NHIF bi Sabina Komba ……aliwataka wafanyakazi
wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi
katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na
kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi
mengi na makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi
No comments:
Post a Comment