Thursday, April 12, 2012

NILIKUWA NAJICHUKIA, HADI VILIVYO KARIBU YANGU- TYSON


Tyson
BONDIA Mike Tyson anajuta, lakini wote tuna majuto. Kitu ambacho hawezi kujutia daima, ni kuwa bondia wa kulipwa.
Katika mahojiano na gazeti la Mirror, Mike amezungumzia show yake ya “Undisputed Truth,” lakini akili yake ni kama mto jinsi unavyoenda.
Kwa sababu gazeti hilo liliandika nchini Uingereza kulaani Tyson alichofanya kabla ya pambano lake na Lennox Lewis.
“Wakati huo napigana na Lennox Lewis,” alisema Tyson, “Nilikuwa ovyo ile mbaya na nilikuwa nafikiri mtu angenipiga bastola. Nilikuwa najichukia na kila kitu kilichokuwa karibu yangu.”
Hayuko ovyo tena na hajichukii tena na yeyote aliye jirani yake. Na wakati Iron Mike yupo nje ya ulingo wa ndondi, ndondi haziwezi kuwa mbali yake, na mtu fulani ambaye anaonekana dhahiri amebadilika.
“Nini David Haye amefanya Munich alipopigana (kavukavu) na Chisora,” Tyson alisema, “hiyo haikuwa nzuri. Huo ulikuwa ni upumbavu ambao niliwahi kuufanya mara awali. Nafikiri kwamba, wakati naangalia hiyo. Hakuna aliyewahi kufanya kama mimi katika kuvunja sheria za ngumi. Haye na Chisora walitakiwa kupinga nilichokifanya. Angalau Haye hajawahi kumng’ata yeyote sikio. Walichokifanya kilikuwa bure.”
Mike alipoulizwa anafikiria nini kuhusu ndondi za uzito wa juu kwa sasa, jibu lake lilikuwa la ajabu.
“Nafikiri ndondi za uzito wa juu ni nzuri sana kwa sasa. Akina Klitschko wanafanya babu kubwa. Si kosa lao kwamba hakuna ushindani wa kutosha.
Lakini sikubaliani na wazo kwamba mabondia wa leo si wazuri kama wa zamani. Kama ungemuuliza Joe Frazier kama angeweza kunipiga wakati nilipokuwa katika kiwango cha juu enzi zangu, angesema, ‘ndio.’ Hivyo ndivyo ngumi zinavyokwenda.
“Nafikiri naweza kuwapiga mabondia wa kizazi kijacho, lakini ukweli wa historia ni kwamba mabondia wanakuwa bora na bora, miili mikubwa na wenye nguvu na nguvu. Nilikuwa na mwili mkubwa kuliko Rocky Marciano na sikuwa mmoja wa mabondia wenye miili mikubwa katika kizazi changu.”
Tyson anafahamu historia ya ngumi, lakini hakuna hakika kama watu watakubaliana na uchambuzi wake. Lakini katika kila maoni yake. Na Tyson, mpende usimpende, msamehe au usimsamehe, lakini amebadilika sana tu.
zaidi tembelea http://bongostaz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment