RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF', Simon Mwakifwamba, ametoa shukrani kwa watanzania wote walioshiriki katika kufanikisha msiba wa aliyekuwa kinara wa bongo movie Steven Kanumba.
Kanumba alifariki Dunia April 7 mwaka huu nyumbani kwake Sinza Vatican na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam April 10.
Akitoa shukruani hizo kwa wandishi wa habari Rais huyo alisema kuwa mbali na wadau wengine pia anamshukuru Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikweti, Makuma wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi na maziri waote walifamnikisha kuzikwa kwa Kanumba.
Hata hivyo alisema kuwa marehemu alikuwa na mchango mkubwa ndani ya TAFF, hivyo kifo cha kimeweka pengo kubwa ambalo haliwezi kufutwa na mtu yeyote.
Hata hivyo alisema kuwa Kanumba alikuwa ni mwanachana wa Shirikisho la Filamu kupitia Chama cha Waigizaji wa mkoa wa Kinondoni, pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu ya kuandaa Mapendekezo ya marekebisho ya kanuna na sheria za filamu za mwaka 2011, pia alikuwa mgadhili wa Shirikisho la Filamu Tanzania
No comments:
Post a Comment