Aliyekuwa
Meneja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Martin Sospeter (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Busness uliopo
Kijitonyama wakati akitoa malalamiko yake kuhusu tuhuma zilizoelezwa
ndiyo chanzo cha kufukuzwa katika bendi ya Twanga majuzi, (kulia) ni
Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa Muzika King Dodoo (kushoto) ni Rais wa
Bendi ya Mashujaa Charles Baba.
****************************************
Akizungumza
na waandishi wa habari Martine, alisema kuwa ''Juzi usiku nilishangazwa
na kauli ya mkurugenzi wangu wa zamani, Asha Baraka, katika taarifa
aliyoitoa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa
amenifukuza kazi kutokana kuihujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki
kujiunga na bendi ya Mashujaa,
Kwa
kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha,
nilimchukulia kama zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa miaka 14
iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya
habari?,
Mimi
sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia
Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku
kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa kuhamia
Mashujaa.
Leo
napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga
na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mkataba wa kazi katika
bendi hii,
“Nilipanga
nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi
kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na
kukubaliana mambo kadhaa na kuona kuwa yana maslahi kwangu,
Mbali
na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na
kunipangishia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa chini ya
Twanga.
Ninaamini
nitafanya vizuri kazi zangu katika bendi hii mpya kama ilivyokuwa
Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo
nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na
hata ninyi wanahabari.
KUNANI WANAMUZIKI WOTE KUTIMKA TWANGA NA KUJIUNGA NA MASHUJAA??
No comments:
Post a Comment