Saturday, May 12, 2012
BONANZA LA TIGO LAFANA SAME
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Tigo imeendesha Bonanza la aina yake katika
viwanja vya Kwasakwasa wilayani Same mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa
na wananchi wengi hususani wanaotumia mtandao huo lengo likiwa ni
kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo mtandao huo.
Akizindua Bonanza hilo Mratibu wa Promosheni kutoka katika kampuni
hiyo,Edwin Shilla alisema lengo la bonanza hilo pamoja na
kushirikishana mambo mbalimbali ya tigo pia wamelenga kutoa huduma
karibu na jamii.
Shila alisema amefurahishwa sana na watu wa mkoa wa
Kilimanjaro ambao walijitokeza kwa wingi katika Bonanza hilo ili kuweza
kufurahia pamoja na kampuni hiyo na kupata huduma mbalimbali za mtandao
huo.
Aidha aliwataka wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na nchini
kote kuendelea kutumia mtandao wa tigo ambao ni nafuu hapa nchini na
unawafika wananchi wote kwa urahisi bila usumbufu.
Akizungumza Ofisa wa Tigo mkoani Kilimanjaro Mohamerd Rajab Bonanza
hili lililenga kuwasogeza kampuni hiyo pamoja na jamii na kwamba pamoja
na maandalizi waliyoyafanya hawakutegemea uwepo wa watu wengi kama
walivyojitokeza.
“Kwakweli Tigo ni mtandao wa watu kwani hatukutegemea umati
mkubwa wa watu namna hii,hasa katika wakati huu ambao kuna hali ya
Mvua,tunawapongeza sana wakazi wa Kilimanjaro hususani wa Maeneo ya Same
na Rombo kwa kujitokezza kuja kushuhudia bonanza hili,tumefarijika
sana”alisema.
Katika Bonanza hilo ambalo kulitolewa zawadi mbalimbali kama
Tishart,Muda wa Maongezi wa Buren a Lain za Tigo,pia lilipambwa na
wanamuziki mbalimbali wa Kizazi Kipya akiwemo H Baba ambaye
alizikonga nyoyo za wanakilimanjaro huku wengi wao wakionekaa
kugombania Tishart ya Tigo aliyokuwa amevaa na Namba yake ya Simu.
No comments:
Post a Comment