Sunday, May 27, 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA


 Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika, zilizofanyika jana, Jijini London Uingereza.
 Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.
 Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
 Kutoka kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George, maarufu kama Queen wa Blog  Uingereza.
 Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London.
***********************************
Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard. 

Aidha Mheshimiwa Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Raisi wa Benin. 

Balozi Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara letu la Afrika.

Kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama Joan Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa nchini Uingereza. 

Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment