Tuesday, May 01, 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
YAH:- MABONDIA WAWILI
WATANZANIA WATINGA HATUA YA ROBO KATIKA MASHINDANO YA KUFUZU
KUELEKEA OLIMPIKI YANAYOENDELEA CASSABLANCA MOROCCO.
Mobondia wa timu ya
taifa waTanzania Selemani Kidunda 69 kgs
welter weight na Emillian Patrick 56
kgs bantam weight wamesonga mbele katika mashindano ya kufuzu kuelekea katika
kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika London Uingereza,katika
mashindano yaliyoanza tarehe 28/4-5/5/2012 Casablanca Morocco.
Mabondia hao wamefika hatua hiyo baada ya kushinda mapambano
yao ya awali kwa seleman Kidunda kumshinda Kab Thiam wa Senegal kwa RSC na
Emillian Patrick kumshinda Tewodros Tilahun wa Ethiopia.
Mabondia hao sasa wamefika katika hatua ya robo fainali
ambapo ni jumla wa mabondia nane waliofikia hatua hiyo na idadi inayotakiwa
kufuzu ni mabondia sita kwa kila uzito.
Mabondia hao kesho tarehe 2/5/2012 watapanda ulingoni kwa
Emillian Patrick kucheza na Isaac Dogboe
wa Ghana na Seleman Kidunda
atacheza na Mehdi Khalsi wa Morocco .
Endapo watashinda watakuwa wameingia hatua ya nusu fainali
na tayari watakuwa wamefikia hatua ya kupata medali ya shaba .
Tanzania ilipeleka jumla ya wachezaji wanne na viongozi
wawili wachezaji wawili Victor Njaiti na Abdalah Kassim walitolewa katika hatua
za awali.
viongozi walioambatana na timu ni Michael Changarawe na Remmy Ngabo.
Aidha kesho kutafanyika mkutano mkuu wa Shirikisho la ngumi
la Afrika (AFBC) Tanzania katika mkutano huo itawakilishwa na makamo wa Rais wa
BFT Michael Changarawe
Kwa niaba ya BFT tunawaomba watanzania wote kila mmoja kwa
imani yake kuwaombea ili washinde na wafuzu
kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa kuzingatia kuwa kwa upande wa ngumi
tulishiriki olimpiki kwa mara ya mwisho mwaka 1996 Atlanta.
No comments:
Post a Comment