Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Kassim Mganga, (kushoto) akiimba katika
jukwaa moja na wanamuziki wa bendi ya Extra Bongo wakati wa onyesho la
bendi hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Meeda uliopo
Sinza Dar es Salaam. Mashabiki wa bendi hiyo walisikika kumshangilia
baada ya kupanda jukwaani na kuimba kipande cha wimbo wa Rejina
Zanzibar, huku wengine wakimtaka kuendelea kuimba bila kushuka jukwaani
hapo.
'Mkaanga Chips' Martine Kibosho, akizicharaza Drams, kwa umahiri mkubwa wakati wa onyesho lao hilo.
Mwimbaji wa Bendi hiyo, Bob Kissa, akiimba jukwaani.
Huyu
yeye ni kiraka katika bendi hiyo, kwani anauwezo wa kuimba, kurap,
kupiga Tumba na kucheza, ambapo ndani ya bendi hii ni Kiongozi wa
Wanenguaji na tayari ametunga wimbo wake utakaokuwa ndani ya albam ya
bendi hiyo ijayo unaokwenda kwa jina la Bakutuka.
Mpiga Gitaa la Besi, mahiri Hosea Bass, akiliungirumisha gitaa katika onyesho hilo.
Wanenguaji
wa bendi hiyo wakishambuliwa jukwaa wakati wa onyesho lao na
kuwapagawisha mashabiki wao ambao kamwe hawakuvumilia kuketi vitini bali
waliamka kila dakika na kwenda kuwatunza.
No comments:
Post a Comment