Wajasiliamali
wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchukua nafasi ya kutangaza bidhaa zao
katika pambano la ngumi la Ubingwa wa Taifa kati ya Rama Kumbele na
James Mokiwa, litakalofanyika Mei 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Vijana
Kinondoni Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com,
mwandaaji wa pambano hilo, T Asenga, alisema kuwa ameamua kutoa nafasi
ya Meza 10 katika ukumbi wa Vijana siku ya pambano hilo ili waweze
kutangaza bidhaa zao kupitia mashabiki na wadau watakaofika kushuhudia
pambano hilo.
Aidha
Asenga alisema kuwa ameandaa meza 10 ambazo Wajasiliamali watatakiwa
kulipia kiasi cha Sh. 100,000/= kila meza ili kuweza kuonyesha biashara
zao ambapo pia watakuwa wakionyesha kupitia Projecta zilizoandaliwa kwa
ajili ya kuonyesha matukio yote ya ukumbini hapo.
Asenga
amewataka wafanyabisharakujitokeza ili kujiandikisha na kuthibitisha
ushiriki wao ili waweze kuingizwa mapema katika orodha ya matangazo.
''Iwapo
wafanyabiashara watahitaji kutangaza ama kuweka matangazo ya biashara
zao katika DVD na kurushwa siku hiyo ya pambano na DVD za mapambano ya
ngumi watatakiwa kulipia kiasi cha Sh. 200, 000/='' Alisema Asenga, na
kiingilio katika pambano hilo ni Sh. 4000 kawaid na 6000 kwa VIP.
KWA MAELEZO ZAIDI WAWEZA KUWASILIANA NA NAMBA ZIFUATAZO:- 0719 546 436/ AU 0684 232 617
Aidha
Asenga alisema kuwa siku ya Mei 12 mwaka huu itakuwa ni siku maalumu
kwa waandishi wa habari kufanya mahojiano na mabondia washiriki katika
kambi zao za mazoezi na kuchukua picha za mazoezi, ambapo amewaasa
mabondia kuwahi na kujiandaa kwa mavazi rasmi ya michezo siku hiyo.
No comments:
Post a Comment