Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana.Picha zote naFather Kidevu Blog
Suma
Lee nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika
wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music jijini Mbeya
Ben
Paul nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuletya raha kwa mashabiki
katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini
Mbeya.
Barnaba
Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani
hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini
Mbeya katika Uwanja wa Sokoine
Vijana wengi walikuwa wamepigilia vitu vya namna hii
Mashabiki walikuwa hawatulii
Mkali
wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani hii wakati wa show maalum ya
Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine
Wasichana waliokuwa wakitoa huduma ya tiketi
Mkali
wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba na Omy Dimpoz katika wimbo Nai Nai
akiimba jukwaani hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music
Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine.Picha zote na Father Kidevu Blog
Dimpoz kwa Pozi akipitika katikati ya wacheza show wake.
Msanii
AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa
show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya katika Uwanja
wa Sokoine jana
Na Father Kidevu Blog, Mbeya.
MANENO
ya Injili yanayosema wa mwisho anakuwa wa kwanza na wa kwanza anakuwa
wa mwisho yametima jana katika Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya pale mkali
wa Hip Hop, Roma Mkatoliki alipoongoza jahazi la wakali wa Tuzo za
Kili Musc Award 2012 katika onesho lao la Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya
jana.
Roma
akipanda juukwaani akisindikizwa na DJ maarufu DJ Choka, alishangiliwa
vilivyo na umati wa watu uliofurika uwanjani hapo pale tu ilipofika
zamu yake kupanda jukwaani.
Roma!
Roma! Roma! Roma!....hayo ndio yalikuwa maneno ya shwangwe kutoka kwa
wapenzi wa burudani kutoka Jijini Mbeya waliofurika katika Uwanja wa
Sokonine mjini hapa kushuhudia show hiyo kali ya Washindi wa Tuzo za
Kili Music Award 2012.
Roma
baada ya kumaliza kuimba nyimbo zake kaza aliwashukuru wana Mbeya kwa
kura zao zilizompa ushindi na kuwaambia sasa anamaliza show hiyo ambayo
hadi hapo alipofikia alisema wametumia Sh 200/= pekee kati ya Sh 2,000
ya kiingilia waliyotoa.
“Sasa
ndugu zangu, nawaambia ukweli hadi sasa mmesha tumia sh 200 tu ya
kiingilio chezu,..sasa nawapa show ya Sh 1,800 iliyobaki,” alijigamba
Roma ambaye muda wote alikuwa akishangilia na ndipo alipomaliza kwa
kuimba Wimbo wa Mathematic uliompa tuzo.
Wasanii
wengine waliopanda jukwaani hii leo ni pamoja na Ben Pol, AT, Ali Kiba
, Barnaba, Omy Dimpoz na Suma Lee nao wamefunika vibaya katika Tamasha
la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa sokoine
Mjini Mbeya.
Alianza jukwaani kupanda mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii Ben Paul
ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae
alishambulia jukwaa na kuwaamsha watu kuwa sasa show imeanza.
Alifuata
jukwaani Suma Lee ambaye aliongozwa na show kali kutoka kwa vijana wake
wane wakike na wakiume na kushangiliwa vilivyo kwa mkongwe huyo wa
Bongo Fleva.
Baada ya Ben
Pol, alipanda mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo
Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT na kutoa burudani ya nguvu na wimbo
wa Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji
wake wawili wa kike.
Ika fika zamu ya
Omy Dimpoz jukwaani kwa kuimba nyimbo yake mpya aambayo alitaraji
kuizindua jana katika Ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam,
single ya Baadae kasha ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa
Kushirikishwa ya Nai Nai aliyo anza kuimba pekeyake na baade kuurudia
wimbo huo akiwa na Ali Kiba.
Ali Kiba alibaki
jukwaani hapo kama ilivyokuwa mjini Moshi na vijana wake kumfuata kutoa
shukrani zao za kupata kura zilizo wapa ushindi wa tuzo ya Wimbo bora
wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa Dushelele.
Wakati mara zote
pazia la utoaji burudani kwa washindi hao wa tuzo za Kili Music Award
2012 wanaofanya ziara limekuwa likifunga na Roma Mkatoliki leo akapnda
wapili kutoka mwisho.
Roma ambaye ni
Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa
Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku
viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka na hata alipomaliza show yake bado
mashabiki walimtaka aendelee.
Mshindi wa Tuzo
ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba ndiye aliyefunga pazia hilo kwa siku
ya leo mjini Mbeya kwa kuimba ikiwapo inayovuma kwa sasa ya Magube
Gube.
Wasanii hao wiki
ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mjini Mtwara na tayari
walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma na
Jijini Mwanza na Moshi
No comments:
Post a Comment