Mkurugenzi
wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ltd,
Henry Machoke (wa pili kulia), akifafanua jambo baada ya kukabidhi
mifuko 100 ya saruji kwa Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dar es
Salaam (Serikali za Mitaa), Method Mkoba (wa tatu kushoto), ikiwa ni
msaada uliotolewa na shirika hilo kupitia kitengo cha huduma kwa jamii
kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wanaoishi katika kambi ya Mabwepande
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kushoto)
ni Mwenyekiti wa Wahanga hao, Khalid Msuya, Meneja Masoko wa NIC,
Adelaida Muganyizi na (Kulia) ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa NIC,
Elisante Maleko. |
No comments:
Post a Comment