Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akipokea DVD maalumu kuhusu Albino na Maisha
yao kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Under the
Same Sun Bi. Vicky Mtetema wakati wa maadhimisho ya Siku ya Albino yaliyofanyika Lindi. Shirika la ni mdau
mkubwa wa watu wenye ulemavu wa Ngozi na linajishughulisha na kutoa elimu kwa
watu wenye Ulemavu wa Ngozi pamoja na Misaada mbalimbali. Spika walikuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani
Lindi Jana.
Dk.
Mashingo Lerise kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Ngozi na Saratani (Ocean Road)
akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) juu ya huduma mbalimbali
zitolewazo na taasisi hiyo kwa watu wenye ulemavu (Albino) baada ya Mhe. Spika
kutembelea banda lao wakati wa kilele cha Siku ya Albino kitaifa iliyofanyika
Lindi. Kulia ni baadhi ya madaktari wa saratani ya Ngozi kutoka taasisi hiyo
katika Hospitali za KCMC na Mkoani Lindi.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Mweneyikiti wa Chama
cha albino Tanzania Ndg. Ernest Kimaya, na Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka
wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ndg. Danford Makala wakipokea maandamano
wakati wa kuadhimisha siku ya Albino Mkoani Lindi ambapo Spika alikuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani
Lindi Jana.
Bi.
Zakia Matimbwa kutoka Albino Revolution Cultural Troup cha Dar es Salaam
akighani Ngonjera iliyobeba ujumbe wa kulaani mauji ya Albino wakati wa katika
maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa
maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana.
Mhe Spika alikuwa Mgeni rasmi katika kilele hicho.
No comments:
Post a Comment