Wachezaji wa St.Agustine wakiwa na furaha
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akimkabidhi Kombe nahodha wa
timu ya St.Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano
ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa
mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA)
Fred Mushi.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji
kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya
Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akizungumza na wachezaji
kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Safari
Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
Wachezaji wa Chuo cha St.Agustine wakiwa wamembeba nahodha wao mara
baada ra Jimmy Nicas kabeba kumbe mara baada ya kuibuka mabingwa wa
Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
CHUO cha St.Augustine cha mkoa wa Mwanza juzi kilitawazwa kuwa
mabingwa wapya wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
yanayojulikana kama 'Safari Higher Learning Pool Competition 2012 baada ya
kuibuka na ushindi wa magoli 13-9 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi chuo cha
IFM kutoka mkoa wa Dar es salaam katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo.
Fainali za mashindano
hayo ambazo zilishirikisha vyuo vinane ambavyo vilikuwa mabingwa katika mikoa
yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo na kudhaminiwa na wadhamini wakuu wa
mchezo wa pool nchini,Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari
Lager,zilifanyikia kwenye ukumbi wa Iringa All Fear mkoa hapa.
St.Augustine kwa kuwa
mabingwa wapya wa mashindano hayo walijinyakulia fedha taslim Sh. Mil.2.5
pamoja na kikombe kikubwa cha ubingwa huo.
IFM ambao licha ya
kucheza vizuri katika fainali hizo na kujikuta wakipoteza ubingwa huo
walizawadiwa fedha taslim Sh.Mil.1.5 kwa kushika nafasi ya pili, chuo cha RUCO
kutoka Iringa chenyewe kiliondoka na Sh.Mil.1.3 kwa kushika nafasi ya tatu na
St.John's kutoka mkoa wa Dodoma kilishika nafasi ya nne na kupewa Sh. Mil.1.
Vyuo
vya MUCCOBS (Kilimanjaro), IAA (Arusha),Mzumbe (Morogoro) na TIA (Mbeya)
vyenyewe vilizawadia Sh.500,000 kila chuo ikiwa ni kifuta jasho cha kushiriki
fainali hizo.
Kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) mchezaji wa chuo cha St. John's cha
Dodoma, Obiara David alitwaa ubingwa huo baada ya kumgaragaza vibaya Jackson
Raphael wa chuo cha MUCCOBS
(Kilimanjaro) magoli 4-0 katika mchezo wa fainali.
Obiara
kwa kutwaa ubingwa huo alijinyakulia fedha taslim Sh.300,000 na ngao wakati
ambapo Jackson kwa kushika nafasi ya pili alizawadia fedha taslim Sh.200,00,
Said Mohamed (RUCO) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.150,000 na Patrick
Peter (IFM) aliambulia Sh.100,000 kwa kushika nafasi ya nne.
Kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Modesta David (IFM) alitwaa ubingwa
huo na kuzawadiwa Sh. 200,000, Remmy Jackson (St.John's) alishika nafasi ya
pili na kupewa Sh.150,000, Suchi Anatasia (KCMC) alishika nafasi ya tatu na
kupewa Sh.100,000 na Violeth Silas (IAA) aliambulia Sh.50,000 kwa kushika
nafasi ya nne.
Aliyekuwa
mgeni rasmi katika fainali hizo ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi.
Wachezaji wa St.Agustine wakiwa na furaha
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akimkabidhi Kombe nahodha wa
timu ya St.Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano
ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa
mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA)
Fred Mushi.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji
kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya
Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akizungumza na wachezaji
kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Safari
Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment