Mmoja wa waandamani wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) Kisiwani Unguja,Zanzibar akionyeshan kitambaa kilicho na Damu mapema leo Asubuhi wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humo,iliyopelekea kuchomwa moto kwa moja ya makanisa pamoja baadhi ya magari yaliyokuwa yameengeshwa karibu na njia wapitazo.vurugu hizo zimeanza jana usiku baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Juimuiya hiyo
Kanisa
la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini
Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana
Gari
la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop
Dickoson Maganga lililochomwa moto usiku wa jana katika eneo la Kariakoo
nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu
shilingi millioni 120.
Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga
lililochomwa
moto na watu wasiojulikana usiku wa leo katika eneo la Kariakoo nje ya
kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi
millioni 120.
Maelfu
ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na
kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama
ilivyofanya Sudan ya Kusini.
Wazanzibari
hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja
vya Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani
Maskani ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya
Lumumba.
Maandamano
hayo walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na
maelfu ya wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa
lililoandaliwa na Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya
Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la
kuzungumzia mfumo wa elimu Zanzibar.
Akizungumza
na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni
matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama
walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao
ndani ya nchi yao.
“Sisi
wazanzibari kama wananchi wengine wowote duniani tuna haki ya kikatiba
kudai nchi yetu kama walivyodai Sudan ya Kusini, mbona Sudan ya
wameweza kujitenda na kupata nchi yao kwa nini sisi kama wazanzibari
tusikubaliwe kudai nchi yetu sasa sisi tunampelekea salam katibu mkuu
wa umoja wa mataifa kumwambia kuwa wazanzibari sasa wanataka nchi yao”
alisisitiza Sheikh Farid huku akiungwa mkono kwa mamia hao kuinua
mikono na kusema ndiooooo.
Awali
Sheikh Farid alisema salamu hizo anataka zimfikie Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Ban Kin moon ambaye kwamba wazanzibari wamechoshwa na
kuwepo ndani ya Muungano ambao umedumu kwa miaka 48 lakini bado ukiwa
na kero nyingi na malalamiko ambayo yanaonekana utatuzi wake ni mdogo
na usiowezekana ambapo alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna
manufaa yena na wazanzibari.
Katika
kuonesha kwamba hawataki tume ya katiba ije kuchukua ya maoni ya
katiba mpya Sheikh Farid alisema wanataka kwanza kuamuliwe suala la
Muungano kabla ya jambo lolote na kuahidi kwamba wataendelea kufanya
makongamano, mihadhara na maandamano kwa kadiri wawezavyo hadi hapo
serikali itakaposikia kilio hicho.
“Ujumbe
huu tunautoa kwa Ban Kin moon, na kwa ulimwengu mzima lakini pia
tunataka rais wetu Dk Shein asikie kilio hiki na Rais Kikwete ambaye
yeye ni mtetezi wa haki za binaadamu na pia ni mfuatiliaji wa nchi
zinazovunja haki za binaadamu tunataka asikie kilio cha wazanzibari
kuwa wanataka nchi yao” alisema.
Alisema
juzi wamefanya maombi maalumu ya kumuombea Rais wa Zanzibar lengo
likiwa ni kumjaaliwa kheri na awe na maamuzi sahihi juu ya wananchi wa
Zanzibar sambamba na kuwaomba Makamu wa Kwanza na makamu wa Pili wa
Zanzibar kusikia kilio cha wazanzibari wasiotaka Muungano.
“Tunamuomba
Rais wetu Dk Shein, Makamu wa Kwanza Maalim Seif na Makamu wa Pili
Balozi Seif kwamba sisi wazanzibari tunahitaji Zanzibar huru,
tunahitaji heshima ya nchi yetu na tupo tayari kwa lolote kwa hivyo
tunataka salamu hizi na ujumbe huu ukufikieni” alisema Sheikh Farid
huku akiungwa mkono na maelfu waliohudhuria katika kongamano hilo
ambalo awali liliandaliwa kwa lengo la kuzungumzia masuala la elimu na
mfumo wake.
Akiendelea
kutoa salamu hizo mara Sheikh Farid alisoma kifungu cha 16 cha katiba
na kuwaleza wananchi kwamba haki ya kutembea ni haki ya kila mwananchi
ambayo imeainishwa katika katiba na sheria za haki za binaadamu hivyo
aliwageukiwa na kuwataka wasimame na kisha kumfuata yeye.
“Haki
ya kutembea ni haki ya msingi kwa mujibu wa sheria na kifungu cha 16
kinatupa haki ya kutembea sasa mimi nataka kutembea jeee mpo tayari
kutembea na mimi? Alihoji Sheikh huyo huku akijibiwa na umma mkubwa
kwamba ndioooo”
Aliongeza
kwamba “Tunaanza kutembea na tuone mtu atukamate tunakwenda njia ya
kinazini, tunapita michenzani, tunapita barabara ya kwa biziredi na
kisha tunarejea hapa hapa kuendelea na kongamano letu kwa amani kabisa
mmesikia….akajibiwa ndiooooo”
baada
ya kusema hivyo Sheikh Farid alitoa takbir na kuanza kukamatana mikono
na viongozi wenzake na huku ummati mkubwa ukiwa umekamatana mikono
nyuma na kuanza safari kwa pamoja na kutembea katika barabara ambazo
walizitaja awali.
Waandamani
hao walikamata mabango yenye maandishi mbali mbali ikiwemo hatutaki
muungano, tunataka nchi yetu, zanzibar bila ya muungano inawezekana na
wengine kadhalika huku wakitembea njiani na kupiga takbir ambapo
walikuwa wakisema Mwenyeenzi Mungu Mkubwa, Mwenyeenzi Mungu Mkubwa sisi
hatuna uwezo isipokuwa tunakutegemea wewe Mwenyeenzi Mungu.
Waandamanaji
hao walianza kutembea kwa utaratibu maalumu huku magari yakisimama na
kuwapisha bila ya kuwepo jeshi la polisi ambapo viongozi wa jumuiya
hiyo na wananchi wengine waliongoza utaratibu huo na kutembea katika
barabara kwa utaratibu mzuri hadi kumaliza maandamano yao waliyoyaita
matembezi ya amani.
Baadae
jeshi la polisi lilifika katika eneo ambalo kumefanyika maandamano
hayo na kufungua mabango yao ya kuwataka watu kuondoka lakini wakati
magari hayo ya polisi matatu yanafika eneo hilo la Kariakoo tayari
ummati mkubwa ulikuwa umeshapita katika eneo hilo na hivyo kuingia
ndani ya magari yao na kuondoka kwa salama.
Awali
akitoa mada katika kongamano hilo, Maalim Abdulhafidh Malelemba
alisema sekta ya elimu imekuw aikidorora Zanzibar kutokana na
kukandamizwa na mambo ya Muungano ambapo kila mwaka wanafunzi
wanapofanya mitihani kufelishwa kwa makusudi huku idadi ya wanafunzi
wanaokwenda katika vyuo vikuu wakiwa kidogo kutokana na kufelishwa
katika mitihani ambapo husainiwa na baraza la mithani Tanzania (NECTA).
Wakizungumza
katika nyakati tofauti katika kongamano hilo, baadhi ya walimu
walisema kukosekana kwa baraza la mitihani Zanzibar kusimamia mitihani
ya elimu ya juu ndio sababu ya wazanzibari kufelishwa kwa wingi na
kushindwa kuingia katika vyuo vikuu kwa kuwa wanafunzi wengi wa
Zanzibar hufelishwa.
Walimu
hao walitoa ushahidi wa hivi karibuni wa kufelishwa wanafunzi wa
kidatu cha nne ambapo walisema lile ni tukio la makusudia lililofanywa
na baraza la mitihani ikiwa ni kuwadhoofishwa wanafunzi wa Zanzibar ili
wasiendelee katika masomo kwa kuwafelisha.
----
----
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 begin_of_the_skype_highlighting +255-777-419473 end_of_the_skype_highlighting / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Tarehe 27MAY2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kila
sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume
Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika
Uislamu.
Jumuia
ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania
wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa
amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume
(S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu,
kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu
(maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa
hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada
(Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.
Jumuia
inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha
amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za
wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya
hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya
inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea
tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea
amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka
kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.
Tunatoa
wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao
kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa
Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya
dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia
haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya
kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
Polisi
na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na
jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya
kulinda haki za wengine.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ .
No comments:
Post a Comment