Mchezaji wa And 1 akifunga katika mechi dhidi ya kombaini ya mkoani Arusha
Mchezaji wa And 1 Chism akipaa hewani kufunga dhidi ya Dar es Salaam
Mwanamuziki Nemless kutoka nchini Kenya akitumbuiza katika tamasha hilo.
Mwanamuziki Ambwene Yesaya AY akifanya viti vyake katika tamasha hilo.
Na Mwandishi wetu
Timu
ya mpira wa kikapu inayoundwa na wachezaji nyota wa zamani wa ligi ya
Chama mpira wa kikapu cha Marekani American Basketball Association (ABA) ijulikanayo
kwa jina la AND1 imemaliza ziara yake kwa mafanikio makubwa huku
ikiacha somo na gumzo kwa Watanzania kutokana na ujuzi walionyesha
katika mchezo huo.
Andi
1 iliyokuwa chini ya mchezaji nyota, Dennis Chism maarufu kwa jina la
Spyda iliweza kufanya mambo makubwa mkoani Mwanza na Arusha baadaye
jijini Dar es Salaam na kuitandika Dar Dream team kwa 123-71.
Mbali
ya Spyda, wachezaji wengine waliokuwepo katika ziara hiyo ni Phillip
Champion Hotsauce, Robert Martin, Marvin Collins Highrizer, Brandon
LaCue Werm, Jamar Davis, Alonzo Miles, Paul Otim na Justin Darlington.
Chism
alisema pamoja na kuwashukuru wauzaji wa kinywaji cha Sprite kwa
udhamini wao na kufanikisha kuja nchini, wamefuraishwa na jinsi
wachezaji wa Tanzania waliovyoonyesha vipaji vyao. Alisema kuwa
wachezaji hao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa na hata
kuweza kucheza ligi za kikapu za kulipwa Duniani pamoja na ile ya NBA.
Mbali
ya kucheza, wachezaji hao walionyesha vipaji mbali mbali walivyonavyo
katika kufunga pointi tatu, ku-dank na staili nyingine ambazo
ziliwasisimua mashabiki wengi.
Baada ya kushiriki katika mechi za mpira wa kikapu, wachezaji hao walijumuika na watanzania wengine katika tamasha la muziki la Coca Cola A Billion Reasons to Believe lililofanyika kwenye ufukwe
wa Mbalamwezi na kuona jinsi gani watanzania walivyokuwa wataalam
katika muziki wa kizazi kipya na hip hop ambao asili yake ni Marekani
ambako wao ndiyo maskani yao.
Wakali
wa muziki kama Ambwena Yesaya (AY) na Nemeless kutoka Kenya walitamba
katika tamasha hilo lililofana na kuwavutia mashabiki wengi.
No comments:
Post a Comment