Monday, May 28, 2012

UZINDUZI NA UTAMBULISHO WA HUDUMA YA AIRTEL SUPER 5 DODOMA


Mnenguaji mahiri wa bendi ya Mashujaa, Lilian Tungaraza ‘Internet’ akiongoza kundi la wanamuziki wa bendi hiyo kulishambulia jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu kwa, Baltazar Theobald, mshindi wa kwanza aliyeweza kueleza vizuri jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa 5 wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Airtel Jiunge na Supa 5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Family, Said Juma ‘Chege’ (kushoto) na Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’wakionyesha makali yao katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mpiga tumba mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica aliyejiunga na bendi hiyo akitokea Twanga Pepeta, Sudi Mohamed ‘MCD’ akionyesha makali yake wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Cyprian ‘ Chaz Baba’ ambaye naye amehama akitokea Twanga Pepeta, akiimba wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Msanii wa kundi la muziki wa bongo fleva la Tip Top Connection lenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam Hamad Ally ‘Madee’ akichengua mashabiki wake waliojitokeza katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Huduma ya SUPA 5 imepokelewa kwa shangwe mkoani Dodoma huku dhamira yake ikiendelea kutimia baada ya umati mkubwa wa vijana kujitokeza ili kufahamu vyema huduma hiyo nafuu iliyozinduliwa wiki moja iliypota kwa lengo la kuwapa unafuu wateja wa Airtel ili kufurahia huduma tano nafuu

Wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha la wazi katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wasanii wa muziki wa Dansi na Bongo Flaver walitumbuiza na kufanya tamasha hilo kufana zaidi

Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye utambilisho wa huduma hiyo mpya kabambe ni pamoja na bendi ya muziki ya mashujaa, kundi la muziki wa kizazi kipya la Tiptop Connection na kundi la Wanaume TMK.

Akitambilisha huduma hiyo mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema, wateja wa kampuni hiyo watapata unafuu mkubwa wa gharama za kupiga simu

“Huduma ya SUPA 5 inamuwezesha mteja wa Airtel kutumia mtandao wa facebook bure masaa 24, kuongea nusu shilingi na watu watatu, kupiga simu kwa robo shilingi kuanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi na kutumia huduma ya internet bure usiku kucha” alieleza Bw, Mmbando

Huduma ya SUPA 5 itaendelewa kutambulishwa katika mikoa mbali mbali kwa kuwa huduma hiyo nafuu ni ya kudumu, mikoa inayotarajiwa kutembelewa kwa kufanyiwa utambulisho rasmi wa huduma hiyo ya Airtel Supa 5 ni pamoja na Morogoro, Iringa, Arusha, Mwanza na DSM.

No comments:

Post a Comment