Thursday, June 28, 2012

Airtel yachangia damu kuokoa maisha ya watanzania


Airtel yachangia damu  kuokoa maisha ya watanzania
Alhamisi, Juni 28 2012, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeandaa
zoezi la kuchangia damu litakalohusisha wafanyakazi wake kuchangia
damu kwa lengo la kuokoa maisha ya  wagonjwa wanaohitaji damu, hii ni
moja  kati ya shughuli za Airtel katika kusaidia jamii

Akiongea wakati wa zoezi la kutoa damu lililofanyika katika makao
makuu ya Airtel Mkurugenzi Rasilimali watu Perece Kirigiti alisema”
Airtel inandeleza dhamira yake ya kusaidia na  kuchangia katika
shughuli za kijamii na leo tunashirikisha wafanyakazi wetu kuchangia
damu katika kukiwezesha kitengo cha  damu salama cha taifa kuwa na
hifadhi ya damu ya kutosha kukidhi mahitaji ya wagonjwa na kuweza
kuokoa maisha ya wagonjwa.
Tutakuwa na zoezi hili siku nzima ya Alhamisi hapa Ofisini makao makuu
Dar es salaam ambapo madaktari kutoka kitengo cha taifa cha kutoa
damu wataendesha zoezi la kutoa damu kwa wafanyakazi na wageni
watakaojitolea kuchangia. Wafanyakazi wetu wanayofuraha kuona wanaokoa
maisha ya watanzania nchini na kwa jinsi hiyo tunatimiza majukumu yetu
katika kusaidia jamii inayotunzunguka
Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamiii bi Hawa Bayumi akichangia
kuhusu jitihada hizi alisema” hii ni moja kati ya jitihada zetu za
kuwawezesha wafanyakazi wetu na wadau mbalimbali kuona jukumu lao
katika kusaidia jamii, na kwa mwaka huu wito ni  changia damu ili
kuokoa maisha”
Zoezi zima la utoaji damu litahusisha kujaza fomu,  mahojiano na
uchunguzi wa afya utakaofanywa kwa kufata kanuni za tiba, kisha
kufatiwa na utoaji damu utakaochukua takribani dakika 10 ambapo
mililita 450 za damu zinategeme kuokoa maisha ya mtu mmoja
Tanzania inahitaji kiasi cha damu cha unit 350,000 kwa mwaka kwa ajili
ya huduma za dharura za tiba ambapo kwa sasa kitengo cha  damu salama
cha taifa kinakusanya unit 115,000- 120,000 kwa mwaka hivyo kuwa na
mapungufu ya kiasi cha unit 235,000.
kitengo cha  taifa cha kutoa  damukitengo cha  damu salama cha taifa
wa damu kwa mwaka huu wa 2012 na kufanya juhudi za kukusanya unit
180,000, hivyo inatoa wito kwa watanzania wenye afya walio na umri
kati ya  18 na 65 na uzito wa 50kgs kuchangia damu ili kuokoa maisha
ya wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu.

No comments:

Post a Comment