Juu ni taswira mbalimbali za Dr. Steven Ulimboka baada ya kuokotwa
Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu Dk Hellen Kejo(kushot)akiwa na Dr. Steven Ulimboka muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha ikulu jijini Dar es
salaam viongozi wa Chama cha madaktari nchini. Wa pili kushoto ni
Mratibu wa mgomo wa madaktari, Stephen Ulimboka na Kulia ni Rais wa
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi
Dr. Steven Ulimboka alipokua akieleza jambo kwenye mkutano wao(madaktari na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Hivi Karibuni
....
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:
Dkt.
Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri
maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe
(Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM,
kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao
ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na
namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa
usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku
wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na
sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
---
UPDATE:
Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------
Baadhi
ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC)
walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania,
Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.
Taarifa
iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata
Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa
kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza
kuzungumza.
Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt.
Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili
wake na anahitaji matibabu ya haraka.
Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.
No comments:
Post a Comment