Wateja wakiwa katika foleni ya kununua
simu aina ya Galaxy Pocket katika duka la wakala wa Samsung
Tanzania jijini Dar es Salaam ambapo wateja
20 wa mwanzo kila mmoja alipata simu za bure
KAMPUNI ya Samsung Tanzania jana imegawa simu 200 bure
aina ya Galaxy Pocket kwa wateja wa kwanza kununua simu hizo.
Promosheni hiyo ya siku moja imekuja baada ya kampuni hiyo
kuzindua simu hizo Juni 14 mwaka huu.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuanza kuuzwa simu hizo na
kutolewa bure, Meneja Mauzo na Usambazaji Kitengo cha Samsung Mobile Sylvester
Manyara alisema promosheni hiyo iliyoendeshwa nchi nzima ilitangazwa kupitia
redio na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Alisema kupitia facebook waliwataka wateja wajitokeze kununu
simu hizo katika maduka ya Samsung ili wapate moja bure, kwasababu ni
promosheni ya siku moja.
“Hii promosheni ilikuwa ni kwa ajili ya wateja 200 tu … kwa
maana tumetoa simu 400; yaani 200 za bure na 200 za kununua,”alisema Manyara
huku akiwashauri Watanzania wanunue bidhaa mbalimbali za Samsung.
Naye Frank Wada mkazi wa Dar es Salaam, aliyenufaika na promosheni
hiyo alisema amefarijika kununua simu hiyo na kupata nyingine bure.
“Unajua kila duka lilikuwa linapokea wateja 20; nilikwenda
duka la kwanza nikakuta kumejaa nikaambiwa waliokuwepo wanatosha ndio nikaja hapa na kupata bahati hii,”alisema
Wada huku akicheka.
No comments:
Post a Comment