Wednesday, June 6, 2012

Kapteni Lusajo Lazaro ahaidi mafanikio zaidi ATCL


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni Milton Lusajo Lazaro.
Na mwandishi wetu 
IKIWA siku mmoja tu baada ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL), Kapteni Milton Lusajo Lazaro amesema shirika hilo linanafasi kubwa ya kupata mafanikio iwapo litaendelea kutekeleza mpango wake wamaendeleo wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, Lusajo alisema atatumia uzoefu wake alioupata katika sekta ya usafiri wa anga kuleta mabadiriko katika shirika hilo na kuliwezesha kushindana sambamba na kampuni nyingine za ndani na nje ya nchi.
Kpt. Lusajo rubani anaeheshimika katika sekta ya usafiri wa anga si kwa Afrika Mashariki pekee ila Afrika kwa ujumla na anarekodi ya kuendesha ndege kwa masaa zaidi ya elfu kumi na mbili na pia amewahi kushika nyadhifa tofauti katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na ATCL kabla ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL.
 “Napenda kutoa shukrani zangu kwa waziri Mwakyembe na viongozi wengine wa Wizara kwa kuwa na imani nami. Nimekubali uteuzi wake na nitafanya kazi alienipa kwa moyo mmoja.
 Nina ahidi kuwa nitautumia uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 35 katika sekta ya usafiri wa anga na kuipa ATCL uwezo kushindana kibiashara. Natoa wito kwa wafanyakazi wenzangu kutoa ushirikiano ilituweze kusonga mbele. ,” alisema.
Lazaro alisema kampuni yake itaendelea kutoa huduma kama kawaida na kuongeza kuwa safari zote za kampuni zitaendelea kama ilivyopangwa na ratiba licha ya mabadiliko ya uongozi.
 “Hakuna sababu ya wananchi kuwa na wasi wasi. Kilichotokea ni mabadiliko ya uongozi tu lakini mipango na shughuli zote za kampuni zinaendelea kama ilivyopangwa,” alisema.
Lazaro aliongeza kuwa jukumu kubwa alionalombele yake ni kuongeza idadi ya ndege za shirika hilo aidha kwa kukodi au kuingia ubia na makampuni mengine katika jitihada za kuimarisha nafasi ya kampuni yake ili iweze kushindana kitaifa na kimataifa katika miaka michache ijayo.
 “ATCL haiwezi kupata mafanikio bila kuwa na ushirikiano mzuri na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla. Nawaomba wananchi waendelee kuonyesha ushirikiano na uzalendo waliouonyesha katika wiki chache zilizopita baada ya kuanza kwa huduma za kampuni yetu.
“Nawahakikishia wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa kampuni yangu itaendelea kutoa huduma na bidhaa bora zilizo katika bei za kiushindani ukilinganisha na makampuni mengine yanayotoa huduma hii katika soko,” alisema.

No comments:

Post a Comment