Ndoto
za Klabu ya Yanga yenye Maskani yake mtaa wa Jangwani jijini Dar es
Salaam za kumtwaa kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tabnzania “Taifa
Stars” Mbrazili, Marcio Maximo huenda zikayeyuka kufuatia kocha huyo
kuwa na mkataba Nchini Brazili.
Katika
salamu zake kwa wana Yanga na watanzania kwa Ujumla Maximo amesema sio
rahisi rahisi tu yeye kuja kuifundisha Yanga kwani bado wapo katika
mazungumzo.
“Ni
kweli nimepokea Mkataba kutoka Yanga, lakini bado tupo katika
majadiliano kwasababu bado nina mkataba hapa, hivyo sio rahisi kuchukua
maamuzi ya haraka”, alisema Maximo.
Aidha
Maximo amesema anajisikia furaha sana na maamuzi ya Clabu ya Yanga
kumhitaji yeye kukinoa kikosi hicho, lakini mbali na Yanga kumhitaji
anasema pia timu kadhaa za afrika zimemhitaji zikiwepo mbili za taifa.
Amezitaja timu zinazomhitaji ni pamoja na St George ya Ethiopia pamoja na timu za taifa za Rwanda na Zimbabwe.
Aidha
Kocha huyo aliyeleta ari ya watanzania kuipenda timu yao ya Taifa na
soka la nyumbani kwa kauli zake za matumini “ Pamoja Tutashinda” amesema
anaendelea kuifikiria Yanga maana uongozi umeonesgha nia ya kutaka
kuiboresha timu.
Mapema
wiki hii, Viongozi wa Yanga walidai kuwa Kocha huyo Mbrazil angewasili
nchini jana tayari kwa kuinona timu hiyo iliyo poteza ubingwa kwa
kichapo cha magoli 5-0 kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Yanga na Kichapo
kutoka kwa wapinzani wao wa karibu Azam kilichopelekea Yanga kuambulia
nafasi ya 3 na kufungiwa kwa baadhi ya wachezaji wake. zaidi tembeleahttp://mrokim.blogspot.com/2012/06/maximo-kuja-yanga-bado-kitendawili.html
No comments:
Post a Comment