Friday, June 1, 2012

MKUTANO WA 29 WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF) WAANZA RASMI NCHINI MAREKANI.


Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani katikati akiwa amesimama na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi wa Tanzania pamoja na promota maarufu wa ngumi wa Thailand Jimmy  Chaichotchuang walipotembelea Pearl Habour tarehe 30 May, 2012.

Mkutano wa 29 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) umeanza rasmi katika Hotel ya Hawaii Hilton Village Resort jijini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 29 May, 2012. Mkutano huu ulianza rasmi saa 3 za asubuhi katika ukumbi wa kimataifa wa Atlatic International Conference Center, kwenye jengo la Rainbow Towers katika hotel hii ya nyota tano.
Tarehe 29 ilianza kwa wajumbe wa mkutano huo kujiandikisha kuanzia saa 3 za asubuhi mpaka saa 11 jioni. Jioni wajumbe wote walikuwa na cocktail party ya get together katika ukumbi wa Rainbow Towers.
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Akiwakaribisha wajumbe walioanza kumiminika katika mkutano huo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani aliwataka wakaribie Marekani na kutumia muda walionao katika jiji la Honolulu kufahamiana na kutembelea jiji hili.
Ratiba ya siku tano itajumuisha kuwa tarehe 29 ni siku ya kuanza kwa mkutano huo kwa wajumbe kujiandikisha. Jioni kutakuwa na party ya kukutana na kufahamiana. Tarehe 30 kutakuwa na ziara ya kutembelea Pearl Habour bandari iliyoharibiwa na majeshi ya Japan mwaka 1941na kuifanya Marekani ijiingize kwenye vita ya pili ya dunia.
Tarehe 31 ni siku rasmi ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani ataufungua rasmi. Wajumbe wengine watakaohutubia ni pamoja na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Wengine ni Lindsey Tucker ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ubingwa wa IBF,  William James ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Viwango wa IBF.
Nao Lou Priluka ambaye ni Katibu wa bodi ya wakurugenzi wa IBF atazungumza pia. Aidha Al Maiyer ambaye ni Mwakamu wa Rais wa IBF atazungumza. Ray Wheatler ambaye anaiwakilisha IBF katika bara la Asia atazungumza.
Rarehe 1 Juni kutakuwa na semina ya Utibabu pamona na Marefari. Tarehe 2 kutakuwa na semina ya Majaji pamoja na programu maalum kwa IBF zitawakilishwa. Mkutano huu utafungwa rasmi tarehe 2 Juni na Mstahiki Meya wa jiji la Honolulu.
Imetumwa toka Honolulu, Hawaii, Marekani na;
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission(TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education and Resources Network (iEARN) to TANZANIA

No comments:

Post a Comment