Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani kushoto akiwa
amesimama na Rais wa IBF bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya
Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi siku ya ufunguzi wa mkutano huo tarehe 31
May, 2012.
Rais Peoplers aliwakaribisha wajumbe na kuwasomea taarifa ya mwaka
ya IBF/USBA ambapo zaidi ya mapambano ya ubingwa 349 yalifanyika chini
ya IBF/USBA mwaka jana.
Mkutano huo ulihutubiwa pia na Rais wa IBF katika bara la Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha
mwakilishi wa IBF katika bara la Ulaya Roberto Reya wa Italia naye
alihutubia mkutano huo.
Katika mkutano huo taarifa ya kifo cha bondia wa Thailkand
Thangthong Kiattaweesuk aliyekuwa na miaka 35 kilitolewa rasmi. Bondia
Kiattaweesuk alikufa katika ajali ya gari akiwa na mkewe, mtoto mmoja na
ndugu yake baada tu ya kushinda pambano lililompa nafasi ya kupigana na
bingwa wa IBF wa dunia katika uzito wa Feather Geoffrey Mathebula wa
Afrika ya Kusini.
Kiattaweesuk alimpiga bondia wa Kenya Geofrey Munica kwa KO raundi ya 10
katika pambano la kugommbea mkanda wa mabara wa IBF.
Pamoja na ufunguzi huo leo kutakuwa na semina ya utibabu pamoja na
semina ya majaji. Mkutano huo utamalizika tarehe 2 Juni.
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani
kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu
maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na
Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
Mtanzania Onesmo Ngowi.
No comments:
Post a Comment