NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
MWENYEKITI wa CCM kata ya Olturument,Thelesia Kitalu anatuhumiwa kuihujumu
bodi ya maji ya kata hiyo,(Meviwasu) kwa kuhamasisha wananchi kungóa
mita za maji zinazofungwa kwenye makazi yao, sanjari na kukata mabomba
ya maji na kujiunganishia kinyemela akiwaeleza kuwa maji hayo ni ya bure
na haifai kuyalipia .
Pia anadaiwa
kufadhili kikundi cha vijana 12 wanaotambulika kwa jina la
‘’Talban’’,ambao wamekuwa na kazi moja ya kungóa mita za mabomba majira
ya usiku na kuendesha vurugu kwa kuwapiga wafanyakazi wa Meviwasu
,wakipinga hatua ya kulipa maji hayo kwa bill huku akiwaeleza wananchi
kuwa shirika la Meviwasu linalojihusisha na mradi wa usambazaji wa maji
vijijini, halipo kisheria.
Add captionHayo
yalibainika jana kati
ka mkutano mkuu wa dharura wa bodi ya maji (Meviwasu)uliofanyika katika
kijiji cha Ilkishini wilaya ya Arumeru,uliowahusisha viongozi wa
kitongoji ,kijiji na kata,madiwani ,askari polisi pamoja na wazee
mashuhuri kutoka vijiji sita vinavyohudumiwa na shirika la Meviwasu .
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa bodi ya maji ,Lomayani Meshurie alisema kuwa lengo la mkutano huo wa dharura ni kujadili hujuma ya ungóaji wa mabomba na mita za maji unaoendelea,ambapo alielekeza lawama moja kwa moja kwa mwenyekiti huyo wa ccm anayedaiwa kuwashawishi wananchi wasikubali kuwekewa mita ili walipie huduma ya maji safi.
Baadhi
ya viongozi wa vijiji na vitongoji waliunga mkono hoja hiyo na
kuthibitisha wazi kuwa mwenyekiti huyo wa ccm ndiye amekuwa akitumia
mikutano yake ya hadhara kuwashawishi
wananchi waukatae mradi huo wa maji ,akidai shirika hilo la Meviwasu
ambalo limetokana na muunganiko wa vijiji viwili vya Muklat na Enaboishu
haliko kisheria.
Shirika la Meviwasu limekuwa likiendesha mradi huo wa maji kwa vijiji saba vilivyomo
wilayani Arumeru,chini ya ufadhili wa shirika la ( Ubu) la nchini
Denmack linalojihusisha kusaidia miradi endelevu ya maji kwa nchi
zinazoendelea.
Mmoja wa wazee
mashuhuri mkazi wa kijiji cha Ekenywa, Mzee Logolie Sailevu alisema kuwa
mwenyekiti huyo amekuwa akihujumu mradi huo kwa lengo la kujipendekeza
kwa wananchili ili kujenga mazingira ya kuchaguliwa katika nafasi ya
uongozi ujao hatua ambayo imesababisha kukwama kwa zoezi la usambazaji
maji kwa wananchi.
‘’huyo mama achukuliwe hatua kali hapa tunao askari polisi ili kushughulika masuala hayo ,amekuwa akiongoza kundi la vijana wa
Talban ili kungóa mita ndio maana vijiji vingi havina maji, huu mradi
umeshindwa kufikia malengo kwa sababu yake ‘’alisema Mzee Logolie huku
akishangiliwa
Akizungumza katika mkutano huo,mwenyekiti huyo anayetuhumiwa, alikiri kulifahamu kundi hilo la Talban na kudai kuwa si
kweli kwamba analifadhili ili kungóa mita za maji ila alisisitiza
kuwaamekuwa na ukaribu na kundi hilo kwa sababu wamekuwa wakimfuata na
kumweleza kero mbalimbali.
No comments:
Post a Comment