Mtayarishaji Mwandamizi wa
Vipindi vya Televisheni wa Shirika la la Utangazaji Tanzania(TBC),
Jeff Shellembi(kulia) akimwonesha Naibu Waziri wa Habari,Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makalla(kushoto) kaseti za kurekodi
habari na vipindi mbalimbali ambayo yenye rangi yekundu na bluu ni
iliyochini ya kiwango ambayo hudumu kwa miezi mitatu na kuathiri utendaji
kazi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo iliyofanyika leo
kwenye kituo hicho cha televisheni cha TBC,Mikocheni jijini Dares
Salaam . Kutoka kushoto wa pili ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Joe
Rugarabamu na aliyevaa kitenge ni Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa
TBC, Suzan Mungy.
Fundi Mitambo wa Shirika
la Utangazaji Tanzania(TBC), Ally Kagomba(kushoto) akimwonesha Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla mitambo
ya ya kurushia vipindi mbalimbali wakati wa Naibu Waziri huyo
alipofanya ziara kwenye kituo cha televisheni cha TBC,leoMikocheni
jijini Dares Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni
na Michezo Amos Makalla (katikati) akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Utangazaji Tanzania( TBC), Wilfred Nyachia baada ya
kumaliza ziara yake katika shirika hilo na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TBC, Joe Rugarabamu.
Waziri Naibu Waziri wa Habari,Vijana,
Utamaduni na Michezo Amos Makalla (katikati) akizungumza na wajumbe
wa Bodi na uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania( TBC),
mara baada kumaliza ziara yake katika shirika hilo.
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.
(Na Concilia Niyibitanga
na Magreth Kinabo – HABARI).
NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,
Amos Makalla ameitaka Menejimenti ya Shirika la Utangazaji la Tanzania
(TBC) na Bodi yake kushirikiana kwa karibu katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendeakazi.
Mhe. Makalla ameyasema hayo leo wakati akizungumza
na Menejimenti ya TBC na Bodi yake katika ofisi za kituo Televisheni
ya Taifa (TBC1) cha Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Waziri Makalla ameiagiza Menejimenti ya Shirika
hilo kutengeneza Mpango Mkakati wa kukabiliana na changamoto pamoja
na matatizo ya Shirika hilo kwa kuzingatia vipaumbele na kuishauri
Bodi ya shirika kuutumia mpango huo.
‘Tengenezeni Mpango Mkakati wa namna ya kutatua
matatizo yanayolikabili Shirika, ili mtoe ushauri kwa Bodi’.
Amesema Makalla.
Aidha, Makalla amekiri kuwa amejionea matatizo na
kuzisikia changamoto zilizopo TBC na ameahidi kuwa Serikali iko bega
kwa bega na Shirika hilo ili kuhahikisha kuwa matatizo hayo na
changamoto hizo zinapatiwa Ufumbuzi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TBC, Bw.
Joe Rugarabamu amesema, TBC inajitahidi kutekeleza majukumu yake
ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii ya Watanzania pamoja
na changamoto ya uwezo mdogo wa kifedha, gharama kubwa za kukusanya
habari, kuzihariri na kuzisambaza kwa Watanzania wote.
Amesema kuwa, Shirika linakabiliwa na tatizo la
uchakavu wa mitambo, gharama kubwa za upanuzi wa usikivu nchi nzima,
uendeshaji wa mitambo hasa ukizingatia kupanda kwa gahrama za umeme
na mafuta na malipo ya wafanyakazi zaidi ya 600.
Bw. Rugarabamu ameongeza kuwa, Shirika halina jengo
moja la kuweka Ofisi za Radio na Televisheni pamoja hali inayofanya
kuwa na sehemu ya Radio, huko Barabara ya Nyerere na Sehemu ya
Televisheni, Mikocheni hivyo kusababisha gharama za uendeshaji
kuwa kubwa.
Naye Mtayarishaji Vipindi Mwandamizi wa
TBC, Bw. Jeff Shellembi amesema, TBC1 inakabiliwa na uhaba wa kaseti
za kisasa kwa ajili ya habari za vipindi vya televisheni , hivyo kujikuta
wakitumia kaseti zilizo chini ya kiwango hali inayosababisha kaseti
hizo kuharibu deki na kuuwa kamera.
Bw. Ali Kagomba ni Fundi Mitambo wa TBC naye
ameeleza kuwa, mitambo mingi ya Shirika hilo ya kurushia matangazo
ni chakavu na mingine ni mibovu kabisa ikizingatia kuwa imeshapitisha
muda wake wa kutumika.
“Kwa Kitaalam na kiufundi mitambo inatakiwa kutumika
kwa miaka si zaidi ya 8, lakini mitambo yetu ina miaka zaidi
ya kumi na huathiri ubora wa matangazo.” Amesema Bw. Kagomba.
Hii ni mara ya kwanza kwa Naibu Waziri, Mhe. Makalla
kufanya ziara ya kikazi katika Shirika la TBC mara baada ya kuteuliwa
kuwa Naibu wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
No comments:
Post a Comment