Monday, June 11, 2012

NMB YAIPA SERIKALI GAWIO LA BILIONI 7.9



Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa  kwa niaba ya serikali amepokea sh 7.9 bilioni kutoka benki ya NMB ikiwa ni gawio  la serikali kwa mwaka 2011 kama ilivoidhinishwa katika mkutano wake mkuu uliofanyika Juni 2, 2012.Gawio hilo lilitokana na serikali kumiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki  ya NMB.
Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo jijini Dar es Salaam Dk. Mgimwa alisema, amefurahishwa  na benki ya NMB kwa utendaji wake kwa kuwa mwaka 2010 iliweza kutoa sh bilioni 5.7 “Benki ya NMB inaonyesha dalili nzuri ya utendaji wake kwa  kuwa ongezeko  hili la mwaka  2011 la sh bilioni 7.9 kwa serikali ni ongezeko zuri na fedha hii iliyotolewa na NMB  Imeweza kuichangia  Serikali baada ya kupata faida kwa kuwa ni nyingi sana na itasaidia kuwalipa wafanyakazi wengi ” alisema Dk.Mgimwa”
Aidha, aliipongez NMB katika juhudi zake za kuisaidia serikali kupitia shughuli mbalimbali za kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya wananchi wenye  mahitaji. Alisema anathamini mchango wa NMB katika ukusanyaji wa kodi unaofanywa kupitia matawi yake yaliyosambaa Tanzania nzimai.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji  wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema  NMB itaendelea kuleta huduma nafuu za kifedha kwa jamii ya kitanzania katika maeneo  yote ya vijijini na mijini “NMB imeweza kufikia wateja wake nchi nzima,pia imeweza kulipa kodi kwa serikali,ndio maana NMB ni benki bora kwa Tanzania
Tukio hilo muhimu lilishuhudiwa na manaibu wawili wa wizara ya Fedha na Uchumi, Katibu mkuu wa wizara ya fedha na manaibu wake watatu, mweka hazina mkuu, wakuu wa wizara zingine pamoja na wafanyakazi wa NMB.

No comments:

Post a Comment