KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake
ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya Darts Mkoa wa Dar
es Salaam yanayotambulika kama “DAR ES
SALAAM DARTS ASSOCIATION TOURNAMENT 2012” yanayotarajiwa kuanza rasmi kesho
Juni 15 na kumalizika jumapili Juni 16,2012, ukumbi wa Moshi Hotel jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam leo, meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
amesema Safari Lager imesaidia kiasi cha fedha kuendesha mashindano hayo ikiwa
ni pamoja na zawadi za vikombe na pesa taslimu.“Safari Lager inaendeleza lengo
lake la kusaidia kukuza zaidi mchezo wa Darts hapa Tanzania’, alisema Bw.
Shelukindo. Safari Lager imekuwa ikidhamini mashindano mbalimbali ya mchezo wa
Darts ikiwa ni pamoja na kudhamini timu ya taifa hapa ndani na nje ya nchi.
Safari Lager imegawa pia vifaa vya michezo kwa maeneo mbalimbali ya kuchezea
Darts Dar Es Salaam na mikoani.
Naye mwenyekiti wa Taifa wa chama
cha Darts cha Taifa (TADA) Bw. Gesase N. Waigama, ambaye pia ni raisi wa
shirikisho la Darts Afrika Mashariki alisema timu shiriki katika mashindano
haya ni Temeke,Ilala na Kinondoni ambazo zimeunda kombania ya Wilala kila
moja.Waigama akiendelea kusema kwamba, “Tunawashukuru sana TBL kupitia bia yake
ya Safari Lager kwa kutupa udhamini mara kwa mara, kwa niaba ya wacheza Darts
tunaahidi kujitahidi kuhakikisha kiwango kinakua na tunafanya vizuri siku hadi
siku kwani hilo ndio lengo hasa la Safari Lager”.
Na kumalizia bwana Shelukindo
alisema, “Tunaendelea kuwashukuru wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, ni kwa
mchango wao ndio na sisi tunaweza kusaidia michezo mbalimbali hapa Tanzania.
Ikumbukwe pia kwamba Safari Lager inasaidia sana katika kukua kwa mchezo wa
Pool kwa sasa, tuna mashindano ya Pool yatakayoanza wiki ijayo na kuendelea
hado Mwezi September, yote haya ni kutokana na mchango mzuri kutoka kwa wateja
wetu na tunashukuru sana kwa hilo”
Katibu wa Chama cha Darts Mkoa wa Dar es Salaam(DADA), Lambart Rwihula akizungumza
Mwenyekiti wa Darts Taifa, Gesase Waigama akizungumza
Picha ya Pamoja ya Meneja wa Safari Lager na Uongozi wa Darts
No comments:
Post a Comment