Meneja Mkuu wa Samsang, Kishoo Kumar (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Simu mpya ya Samsung
Galaxy Pocket Dar es Salaam .Kushoto ni Meneja mauzo wa Samsug, Sylivester
Manyara
Meneja
mauzo wa Samsug, Sylivester Manyara(kulia)akimkabidhi zawadi ya simu mpya ya
Samsang Galaxy Pocket Mhariri wa makala
wa Gazeti la Tanzania Daima, Amana Nyembo baada ya kushinda droo ya bahati na
sibu kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu hiyo Dar es Salaam
KAMPUNI ya SAMSUNG Tanzania leo imezindua rasmi simu yake
mpya aina ya Smartphone inayojulikana kama “Samsung
Galaxy Pocket”. Uzinduzi huo uliofanyika mbele ya waandishi wa habari
jijini leo.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bwana
Kishor Kumar alisema, “simu yetu ya Samsung
Galaxy Pocket ndio simu ya aina ya Smartphone inayopatikana kwa bei nafuu
zaidi kwa sasa hapa Tanzania. Simu hii inampatia mnunuzi thamani halisi ya pesa
zake kwani inauzwa kwa shilingi 199,000/=
pekee na inakuja ikiwa na offer nyingine nyingi kama simcard na airtel bundle
za zawadi”.
Naye Meneja
Mauzo na Usambazaji wa kitengo cha Samsung Mobile kwa Tanzania Bwana Sylvester
Manyara, aliongeza kwamba “simu zetu za Samsung
Galaxy Pocket zitapatikana madukani zikiwa zimeshaunganishwa na offer aina
tatu. Offer ya kwanza ni simcard ya mtandao wa airtel, offer ya pili ni
Internet bundle ya 250 MB kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe ya
kwanza ya manunuzi. Offer ya tatu ni SMS 100 kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja
kama ilivyo kwa internet bundle”.
Wakiongea kwa
nyakati tofauti baadhi ya wateja walisifia sana simu hii mpya kwa urahisi wa
kutumia na Application zake za ajabu. Bwana Gerald Simbo, Mwanachuo wa IFM
alisema “Simu hii ina uwezo wa Multi
Task yaani inamuwezesha mtumiaji kufanya shughuli zaidi ya nne, hii ina
maana unaweza kuwa unaongea na simu, unatumia mtandao wa Facebook nk. Napenda
pia uwezo wake wa kuhifadhi miziki kwenye Pocket
Music”. Naye Bwana Enock Kweka mwanachuo wa UDSM alisema, “Application
ninayoipenda sana mimi ni Find My Mobile,
hii inaniwezesha kujua simu yangu ikipotea naweza kuipata wapi, hii ni kwa
msaada wa Samsung ambao wanaweza kuiona katika system zao”. Bi Belinda Lawuo
ambaye ni mwanachuo wa CBE alisifia uwezo wa Samsung Galaxy Pocket inavyoweza
kufukuza mbu usiku inapowekwa kwa kutumia application yake ya Mosquito Repellant. Bi Grace Kijo,
Designer wa mavazi na mwanachuo wa chuo cha SJMC alisema, “Application mpya
ambayo iko kwenye simu hii na naipenda ni Swipe,
application hii inaokoa muda kwani sina haja ya kuandika neno zima wakati wa
kuandika, nagusa tu baadhi ya herufi na neno linajiandika lenyewe mara moja”.
Bwana Manyara
alimaliza kwa kusema, “Tunawashukuru watanzania kwa kutuunga mkono kwa muda
wote, tumewaletea zawadi hii wafurahie, inapatikana katika maduka yote kwa
sasa, tuna matangazo redioni, katika television, mabango ya barabarani na
tunawaomba kutembelea website ya simu hii galaxypocket.co.tz
na facebook page ya simu hii facebook.com/pages/Samsung-Galaxy-Pocket”.
Meneja
mauzo wa Samsug, Sylivester Manyara(kulia)akimkabidhi zawadi ya simu mpya ya
Samsang Galaxy Pocket Mwandishi wa habari wa Chanel ten,Shadrack Pete kwa niaba ya Fred Mwanjala, Amana Nyembo baada ya kushinda droo ya bahati na
sibu kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu hiyo Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment