Kalala Junior, akiwa katika mazoezi ya mpira wa Kikapu na timu yake ya Oilers, yanayofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club.
Kalala Junior |
MWIMBAJI
mahiri na mmoja wa Wakurugenzi wa bendi ya Mapacha wa3, Kalala Junior,
amesema kuwa yote yanayosemwa na baadhi ya watu na yanayoandikwa na
baadhi ya vyombo vya habari yamekuzwa tofauti na ukweli kuhusu kupumzika
kwake katika bendi hiyo.
Kocha wa Kalala, Mziray Kinje |
Siku
chache zilizopta Kalala, aliripotiwa kuipa kisogo bendi yake hiyo, kwa
kile kilichoelezwa kutokea mtafaruku wakutoelewana na mwenzake Jose Mara
na Mpiga Solo wao, Allan Kiso Mundele, huku ikielezwa kuwa mapacha hao
waili Jose na Kalala walifikia hatua ya kushikana mashati wakitaka
kuzichapa kavukavu.
Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, umezungumza na mkali huyo Kalala Junior, ambaye ameamua kufunguka na kuweka
wazi ukweli kuhusu jambo hilo na tukio lenyewe linaloelezewa tofauti.
Sufianimafoto,
alikukutana na Kalala, katika foleni ya magari eneo la Kituo cha
Studio, na mafoto ilipojaribu kumdadisi Kalala, alisema kuwa asingeweza
kuzungumza kwani alikuwa akiwahi kwenye mazoezi ya Mpira wa Kikapu na
timu yake ya Oilers, inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza ngazi ya Mkoa wa
Dar es Salaam, inayojifua katika Viwanja vya Leaders Club.
Mafoto,
iliamua kugeuza gari na kuongozana na Kalala, hadi Leaders ili kujua
kulikoni, mkali huyu kuamua kuacha muziki na kujikita katika mchezo wa
mpira wa Kikapu.
Baada
ya kufika katika viwanja vya Leaders, Mafoto ilimshuhudia Kalala,
akijumuika na wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Oilers, huku wakiongozwa
na Nahodha wa timu hiyo, ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa ya
Mpira wa Kikapu, Lusajo Samwel, huku timu hiyo ikiwa ni chini ya Kocha
wake, William Mziray 'Kinje'.
Kalala,
alisema kuwa timu yake hiyo iko katika mazoezi makali ya kujiandaa na
mchezo wake dhidi ya timu ya Magone, mchezo utakaochezwa siku ya
jumapili saa sita mchana Uwanja wa ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mtandao huu, Kalala, alisema kuwa amekuwa akisikia mengi kuhusu kupumzika kwake jambo ambalo amesema si kweli.
Akifungika
zaidi Kalala, amesema kuwa yeye ameamua kupumzika kwa kipindi cha mwezi
mmoja na nusu baada ya kujihisi kuchoka kwa kufanya kazi kwa muda mrefu
bila kupumzika, kama ambavyo alifanya Jose Mara siku za hivi karibuni.
''Mimi
nimeamua tu kupumzika kwani nimechoka na nimefanya kazi kwa muda mrefu
bila kupumzika, hayo yanayosemwa na watu wala si ya kweli, mimi na Jose
tulitofautiana tu katika mazingira ya kazi wala hatukupigana kama
inavyoelezwa, kama unavyojua mimi ni kiongozi katika bendi sasa
inapotokea mwenzio amekosea ni lazima kumweleza ukweli na ndiyo
iliyotokea, kwani kama unavyofahamu mtu unapokuwa tayari damu imechemka
huwezi zungumza taratibu, basi watu wakahisi tunagombana jambo ambalo si
la kweli,
Na
pia sijagombana na wenzangu, nasisitiza kuwa nimeamua kupumzika na
nitakapokamilisha siku zangu za mapumziko nitarejea kazini kama kawaida,
na juzi tu nimezungumza na wenzangu na wanatambua mapumziko yangu, hao
wanaosema nataka kwenda Twanga, sijui Mashujaa, mara Extra Bongo, ni
wazushi tu, sina mpango wa kufanya hivyo na iwapo itatokea kufanya hivyo
basi ni mimi ndiye wa kutoa taarifa hizo,
Katima
muda wangu wa mapumziko nimeamua kujishughulisha na kujiweka bize na
mazoezi ya Mpira wa Kikapu, wala si kweli kuwa nimeamua kuacha muziki na
kuamua kucheza kikapu, haya ni mazoezi tu ikiwa ni pamoja na kutafuta
pumzi zaidi''. alisema Kalala
Kalala (katikati) akiwa katika mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya Oilers.
Kalala (katikati) akiwa katika mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya Oilers. zaid tembelea http://sufianimafoto.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment