Sunday, June 24, 2012

SIMBA YAITWANGA TOTO 2-0 DIMBANI CCM KIRUMBA


Kikosi cha Simba leo dimbani CCM Kirumba kutoka kushoto ni Abdullah Juma, Amri Kiemba, Haruna Shamte, Salim Kinje, Hassan Kondo, Haroon Othman, Paul Ngalewa, Abdallah Seseme, Uhuru suleiman, na Obadia Mungusa. Aliyesimama mbele ni golikipa Hamadi Waziri.

Kikosi cha Toto Africans leo dimbani CCM Kirumba.

Waamuzi wakiwa na manahodha wa timu zote mbili.

Benchi la timu ya Simba, Kaseja akiwa kwenye benchi (mwenye head phone).

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akisalimiana na wachezaji wa Simba.

Mkuu wa mkoa akitoa nasaha kwa timu za Toto na Simba kabla ya kuanza kwa mpambano wa kirafiki katika uwanja wa CCM Kirumba huku akiwa na viongozi, kushoto kwake ni mwenyekiti wa MZFA Jackson Songora,  mkuu wa wilaya ya Kwimba Suleiman Mzee na kulia kwake ni Omar Juma ambaye ni kamisaa wa mchezo huu na mjumbe wa TFF Samwel Nyala.

Salaam kabla ya mchezo.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akiwa na Jack Fish pamoja na Mjumbe wa TFF Samwel Nyala wakifuatilia mpambano wa kirafiki baina ya Simba na Toto Africans ya Mwanza.
Upande wa jukwaa la mashabiki wa wekundu wa Msimbazi wakishangilia baada ya kupata goli kipindi cha kwanza lililofungwa na Uhuru Selemani.

Wadau na pesa zao jukwaa kuu wakiongozwa na Mc Maarufu jijini Mwanza Mc Bonke.  
Goli la pili la Simba limepatikana kipindi cha pili kupitia mchezaji Salim Kinje.

Hadi mwisho Simba 2 Toto 0.

No comments:

Post a Comment