Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp,
Hussein Mbululo (kulia) akipokea Tuzo ya utoaji bora wa huduma
ijulikanayo kama ‘Century International Gold Quality ERA Award’, kutoka
kwa Rais na Afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Kimataifa ya Business
Initiative Directions, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi. Twiga Bancorp
imepata tuzo hiyo,kwa utoaji huduma zinazoridhisha kwa wateja, Uongozi
bora, Mipango mkakati inayokidhi haja ya wateja kama inavyotambulika
katika QC 100 TQM.
Hivi karibuni Benki hiyo ilitunukiwa
Tuzo ya Dhahabu iliyotolewa na jijini Geneva Uswis, tuzo hiyo
inajulikana kama Century International Gold Award (ERA).
Lengo la tuzo hiyo ni kutambua ubora wa
huduma zitolewazo kwa wananchi na taassisi au kampuni mbalimbali lengo
lokiwa ni kuhamasisha utolewaji wa huduma bora kwa wateja.
Mtendaji Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo,
Hussein Mbululo amesema kwamba Benki yake ilikuwa miongoni mwa Benki
100 zilizoshinda katika tuzo hizo kutoka nchi 47, tuzo hizo ziligawanywa
katika makundi saba.
Amesema kujituma miongoni mwa wafanyakazi katika kuwahudumia wateja pamoja na ubunifu ndio siri kubwa ya mafanikio.
Twiga Bancorp ni Benki inayo milikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%).
Afisa Mtendaji wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akiwa na baadhi ya maofisa wa BID mjini geneva kabla ya kuanza utoaji Tuzo.
No comments:
Post a Comment