Wabunge
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika
madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.
Wabunge
hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo
safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana
Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge
wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo
hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge
EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose
SaddrudinBhanji.
Wengine
ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo
Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi,
Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa
wake wa Uwaziri.
Wabunge hao wameapisha pamoja na
wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na katika picha juu ni Waziri
wa Afrika Mashariki na mbunge wa Urambo Mh Samwel Sitta akiapa katika
bunge hilo jana jijini ArushaSOURCE: FATHER KIDEVU BLOG
Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo chake
Mh. Alhaji. Adam Kimbisa
Mhe. Anjela Charless Kizigha
Mhe Bernard Musomi Murunyana
Mh.Abdullah Alli Hassan Mwinyi
Mh.Nderkindo Perpetua Kessy
Mh.Charles Makongoro Nyerere
Dkt Twaha Issa Taslima
No comments:
Post a Comment