Mmoja wa wakazi wa Iringa aitwaye Theresia
Mifwa akikabidhiwa simu ya mkononi aina ya sumsung na Meneja Mahusiano
wa Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando, mara baada ya kuichambua vyema
huduma ya Jiunge na Supa5 kwa ufasaha ,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya
ya Airtel Jiunge na Supa5 uliyofanyika jana kwenye uwanja wa Mwembe
Togwa mkoani Iringa. Airtel Jiunge na Supa5 Ilizinduliwa kwa mara ya
kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Ukitaka kujiunga na huduma
hiyo ANDIKA SMS YENYE NENO ‘WIKI’ AU WIKI UTUME KWENDA 15548.
Kundi la wasani mahiri wa muziki wa kizazi
kipya,lenye maskani yake Temeke,jijini Dar liitwalo Wanaume
Halisi,likiongozwa na Sir Juma Nature,wakilishambulia jukwaa vilivyo
jana jioni mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi
kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,mjini humo na kushuhudia uzinduzi wa
huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za
huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo itaendelea
kutambulishwa tena katika mkoa wa Arusha na baadaye jijini Mwanza.
Wakazi mbalimbali wa mjini Iringa
wakiendelea kuhamia Airtel na kujipatia huduma mbalimbali zilizokuwa
zikipatikana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye
lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel
kwa wateja wake.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya
(hip hop), aitwaye Roma akiwarusha baadhi ya Wakazi wa mji wa Iringa
walijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,mjini humo na
kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa
huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo
itaendelea kutambulishwa tena katika mkoa wa Arusha na baadaye jijini
Mwanza.
No comments:
Post a Comment