Saturday, June 16, 2012

WATOTO WATAKA WAWEKEZAJI MKUNUNA MAGARI KWA AJILI YA WANAFUNZI



 
NA MWANDISHI WETU ALIYEKUWA KISARAWE
BAADHI ya watoto nchini wameitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Inayoongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba, kuweka kipengere katika Katiba Mpya kitakachowalazimisha wawekezaji kununua magari kwa ajili ya  wanafunzi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Fullshangweblog, Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani leo, wakati wa maandhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika,  ikiwa  ni kumbukumbu ya mauaji ya
watoto yaliyofanywa na utawala wakibaguzi Katika Kitongiji cha Soweto nchini Afrika Kusini mwaka 1976  wanafunzi hao wa Shule ya Sekondari Makurunge  walisema sheria hiyo inawezekana iwapo viongozi watakuwa na dhamira ya kweli.
Walisema kwa kuwa katiba ndio muongozo wa kila nchi hivyo wanaamini kuwa kipengere hicho kitakapoingizwa kitawaongoza wawekezaji wenye nia ya kweli ya kuwekeza nchini kufuata sheria hiyo.
Mmoja wa wanafunzi hao, Sharifa Haroun ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo alisema sheria hiyo inawezekana kwani zipo baadhi ya nchi kama Botswana inacho kipengere hicho katika Katiba yake.
Alisema kutokana na sheria hiyo nchini humo, wanafunzi wake wamekuwa wakienda shuleni kwa kutumia magari yaliyonunuliwa na wawekezaji bila usumbufu.
Naye Mwantumu Nassoro alisema sheria hiyo, itaangalia uwezo wa kila mwekezaji kisha kupangiwa kiwango chake cha ununuaji wa magari hayo ya wanafunzi kwa mfano kuana atakayeweza kununua 100, 200, 300 na wengine zaidi.
“Unajua hivi vitu vinawezekana ikiwa viongozi wa nchi hii wataamua na tunatoa tahadhari kuwa haya ni maoni karibu ya wanafunzi wote hivyo tunawaomba wasimamizi wa Tume wayachukuwe na wayafanyie kazi”alisema Mwantumu.
Mwanafunzi mwingine, Mwajuma Idrissa yeye alisema umefika wakati kwa viongozi na wadau wengine kukumbuka zaidi maslahi yao zinapotokea fursa kama hizi zinazo nchi kwa ujumla.
Alisema wanataka mchakato unaoendelea wa upatikanaji katiba mpya lazima utowe nafasi kwa watoto kuchangia kile wanachoona kitawasidia katika kuwaondolea kero zinazo kwamisha jitihada zao za kujipatia elimu bora.
Aidha, Mwajuma aliongeza kuwa, katika hilo la wawekezaji kununua magari ya wanafunzi ni kwamba gari hizo itawalazimu kuzisimamia katika matengezo kila yanapohitajika ambapo serikali itahusika katika kuyapangia maeneo ya kufanya kazi hiyo nchini. Kwa habari zaidihttp://www.fullshangweblog.com/

1 comment:

  1. Usually I don't read post on blogs, but I wish to say that this write-up very pressured me to take a look at and do it! Your writing taste has been amazed me. Thanks, very nice article.

    Here is my site cellulite treatment reviews

    ReplyDelete